UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unafanyika mchana huu kwenye Ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam.
Mchuano
mkali unaelezwa upo katika nafasi ya rais, ambapo wagombea Athuman
Nyamlani na Jamal Malinzi wanachuana vikali kumrithi rais wa sasa wa
TFF, Leodegar Tenga anayemaliza muda wake.
Wagombea
wengine katika uchaguzi huo ni kama ifuatavyo; Imani Omari Madega,
Ramadhan Omar Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais).
Kwa
upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kalilo Samson (Kanda namba
1- Geita na Kagera), Jumbe Odessa Magati, Mugisha Galibona, Samwel
Nyalla na Vedastus Lufano (Kanda namba 2- Mara na Mwanza), Epaphra Swai
na Mbasha Matutu (Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu).
Ali
Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali (Kanda namba 4- Arusha na
Manyara), Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo (Kanda namba 5- Kigoma
na Tabora), Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo (Kanda namba 6-
Katavi na Rukwa), Ayoub Shaibu Nyenzi, David Samson Lugenge, John
Exavery Kiteve, Lusekelo Elias Mwanjala (Kanda namba 7- Iringa na
Mbeya).
James
Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge (Kanda namba 8- Njombe na
Ruvuma), Athuman Kingombe Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee
Damoder (Kanda namba 9- Lindi na Mtwara), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart
Ernest Masima, Charles Komba (Kanda namba 10- Dodoma na Singida), Farid
Nahdi, Geofrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala) na
Twahil Twaha Njoki (Kanda namba 11- Morogoro na Pwani).
Davis
Elisa Mosha, Khalid Abdallah Mohamed (Kanda namba 12- Kilimanjaro na
Pwani), Alex Crispine Kamuzelya, Kidao Wilfred Mzigama, Muhsin Said
Balhabou na Omary Isack Abdulkadir (Kanda namba 13- Dar es Salaam).
Wawakilishi
kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ashford
Mamelodi ambaye ni Ofisa Maendeleo wa kanda hii, Magdi Shams El Din
ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na Rais wa Chama cha Mpira
wa Miguu Zanzibar (ZFA) ni miongoni mwa wageni watakaohudhuria mkutano
huo.
0 comments:
Post a Comment