Nukuu ya kilichoandikwa:
Wanafunzi wa UDom College of Health Sciences, School of Medicine ambao wako clinical years (mwaka wa nne na mwaka wa tano) hawajafungua chuo bado na hawajui ni lini watafungua.
Hata hivyo wanafunzi wanalalamika kua hata upatikanaji wa waalimu imekua ni shida hivyo kufanya mafunzo yao kwa
vitendo kua magumu sana hasa katika miaka hii miwili ya masomo. Hii inawatia hofu sana wanafunzi ambao wako mwaka wa mwisho ambao wanatazamia kumaliza taaluma yao na kujiunga na internship hasa ukizingatia kwamba internship ni zoezi la kitaifa (halina excuse na ratiba mbovu za chuo).
My take; JK, UDom ikitoa madaktari wabovu ni janga kitaifa, ni hasara kwa Serikari, vilevile ni aibu kwa vyuo vya Serikari, utawala pale central kuna uzembe/matatizo, chukua hatua wanafunzi hawa warudi shuleni kumalizia taaluma zao na suala la waalimu vilevile lipatiwe ufumbuzi!
Nawasilisha!!
---
by maghambo619
via JF: News Alert: Jk unajua kinachoendelea udom skuli ya tiba?
0 comments:
Post a Comment