Tuesday, 22 October 2013

RENAMO WASHAMBULIA POLISI MSUMBIJI

 
Afonso dhlakama wa chama cha Renamo

Ripoti kutoka Musumbiji zinaarifu kuwa wanaharakati waliojihami kutoka kundi la upinzani la Renamo,wameshambulia kituo kimoja cha polisi katika mji wa kati wa Maringue.

Kisa hicho kinajiri siku moja baada ya Renamo kusema kuwa inajiondoa katika mazungumzo ya amani ya mwaka 1992 yaliosababisha kusitishwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
    
Renamo ilikaidi makubaliano hayo baada ya vikosi vya serikali kushambulia kambi iliokuwa na kiongozi wake Afonso Dhlakana na kumlazimu kutoroka.
Hali ya wasiwasi kati ya serikali na Renamo imeongezeka katika siku za hivi karibuni huku mapigano yakiripotiwa katika maeneo mbalimbali.

  Inakadiriwa kwamba zaidi ya watu milioni moja waliuawa katika vita hivyo vya miaka 16 vilivyosababisha mazungumzo ya amani huku Renamo ikibadilika kutoka kundi la wanamgambo hadi chama cha kisiasa.

0 comments: