Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini
Njombe jioni ya Alhamisi, Oktoba 17, 2013, kuanza ziara ya wiki moja
kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Njombe.
Miongoni mwa shughuli kubwa ambazo Rais Kikwete atazifanya katika ziara hiyo, ambayo ni yake ya kwanza tokea Njombe itangazwe kuwa Mkoa, ni kuuzindua rasmi Mkoa huo.
Katika siku yake ya kwanza, Ijumaa, Oktoba 18, 2013, mbali na kuzindua Mkoa wa Njombe pia atazindua Kiwanda cha Chai katika eneo la Ikanga na kuzungumza na wananchi.

Rais Kikwete atatembelea wilaya zote za mkoa huo ambazo ni
Njombe, Wanging’ombe, Ludewa na Makete, pia atazindua Chuo cha VETA cha
Mkoa. Aidha, Rais atatembelea na kupata taarifa kuhusu maendeleo ya
mradi wa chuma wa Liganga.
0 comments:
Post a Comment