WENGER: ‘WANAO WACHEZAJI WAKUBWA, UZOEFU MKUBWA NA NI KLABU KUBWA!’
Baada ya Mechi 8, Man United wapo Nafasi ya 8 na huu ni mwanzo mbovu kabisa kwao kwenye Ligi katika Miaka 24.
Wenger amesema: “Je Man United wako nje ya mbio za Ubingwa? Hapana, lakini ingekuwa Pointi 10 lingekuwa ni pengo kubwa kidogo!”
Aliongeza: “Wao wana Wachezaji wakubwa, wenye uzoefu mkubwa na ni Klabu kubwa!”
Juzi Jumamosi, Bao la Dakika ya 89 la
Adam Lallana wa Southampton liliwanyima Man United ushindi walipotoka
Sare 1-1 na Southampton kwenye Mechi ya Ligi iliyochezwa Uwanjani Old
Trafford.
Siku hiyo hiyo, Arsenal waliitwanga Norwich City Bao 4-1 na kukaa kileleni wakiwa Pointi 2 mbele ya Chelsea.
Wenger ametamka: “Ukiwa na chaguo,
utataka uwe kwenye mbio juu kileleni, lakini leo hii huwezi kuwaondoa
Man United! Ni mapema mno! Ni gemu 3 tu na Msimamo unabadilika!”
Man United walianza Ligi kwa kuichapa
Swansea Bao 4-1 na wametoka Sare mbili na Chelsea na Southampton
kuzifunga Sunderland na Crystal Palace lakini wamefungwa na Liverpool,
Manchester City na West Brom.
0 comments:
Post a Comment