Wednesday, 2 October 2013

DK SLAA ANAENDELEA NA ZIARA YAKE YA KUTAFUTA UFUMBUZI WA TATIZO LA KIUCHUMI

Picture
Dk Slaa katika picha ya pamoja na Wakuu wa mashirika makubwa yanayotengeneza mashine nzito za ujenzi na viwanda.
 
Asubuhi ya siku ya Jumanne, Oktoba Mosi, 2013, Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Dk Wilbrod Slaa kutoka Washington DC alielekea kwenye jimbo la North Carolina ambako alilakiwa na Rais wa Chuo cha Piedmond Community College, chenye jumla ya campuses 16 na jumla ya wanafunzi 85,000.

Piedmont Community College ni moja ya Community Colleges bora zaidi nchini Marekani, na imekuwa ikitayarisha wanafunzi mahiri kwenye eneo la uhandisi.

Lengo kubwa la kiongozi huyu maarufu nchini Tanzania kukutana na Rais wa Chuo hicho, ni kujifunza siri ya mafanikio ya
 Chuo hicho, kwa ajili ya kupata mbinu mbadala za kuwawezesha wanafunzi wa Kitanzania kufanya vizuri zaidi kwa lengo kubwa la kutayarisha rasilimali watu. Dk. Slaa pamoja na CHADEMA, wanaamini kwamba, ili kuliokoa Taifa, ni lazima elimu ipewe nafasi ya kwanza.

Kadhalika, Dk Slaa na Rais was chuo kikuu cha Pedmont walikubaliana kuanzisha programu maalum itakayowawezesha vijana wa Kitanzania na wa Kimarekani kuanzisha urafiki utakaoziwezesha chuo hicho maarufu kufanya kazi kwa ukaribu na vyuo vya Tanzania. Vyuo vya Kitanzania vitaweza kunufaika zaidi hasa kutokana na teknologia ya kipekee ambayo hipo chuoni hapo.

Baada ya kumaliza ziara katika chuo cha Central Piendmond, Dk Slaa alikutana na Wakurugenzi na viongozi wengine wakubwa wa mashirika makubwa ya uhandisi kama vile Caterpillar, Freightlighner, Siemens, Cummings na mengineyo ambayo yanatengeneza zana nzito "Heavy Equipmets" zinazohitajika nchini Tanzania ili kuboresha miundombinu yetu.

Viongozi hao walifurahishwa na mikakati na sera za CHADEMA za kuwavutia wawekezaji. Walifurahishwa sana pia na ahadi ya Dk Slaa ya kukomesha ufisadi ambao ndiyo tatizo kubwa linalowakwamisha wawekezaji wa kigeni nchini.

Dk Slaa amemaliza ziara yake jimboni North Carolina kwa kukutana na Wawuu wa Charlotte Chamber of Commerce. Walijadiliana mambo kadhaa ikiwemo kusaidiana kutafuta wawekezaji ambao wataleta biashara isiyo kandamizikati ya makampuni kutoka North Carolina na Tanzania.

Baada ya miaka 52 ya ufisadi na kuuzwa kwa rasilimali za nchi, elimu duni, umasikini wa kupindukia, huku taifa likiendelea kuwa ombaomba Dk Slaa na CHADEMA wameamua kutafuta njia mbadala ya kuleta ukombozi karibu na wananchi. CHADEMA imeanza kutafuta mbinu za kumkomboa Mtanzania kutoka kwenye ufukara lengo likiwa ni kutengeneza mamilioni ya ajira ambazo makampuni mengi yako tayari kuyazalisha kama CHADEMA itatengeneza mazingira mazuri ya kuwekeza.

Dk Slaa amemaliza ziara ya siku moja katika jimbo la North Carolina na kuondoka kuelekea jijini Atlanta, Georgia ambako atakutana na viongozi wa shirika la Coca-Cola, AT&T pamoja UPS.

--- Imeandikwa na Rtackket
 

0 comments: