Thursday, 23 January 2014

AJARI YAOKEA: AFA KWA KUGONGWA NA GARI MKOANI IRINGA


RPC MUNGI.
Mtu mmoja mkazi wa Mbalamaziwa wilaya ya Mufindi Bw Traifon Mpiluka (55)  amefariki dunia baada ya kugongwa na gari eneo la barabara kuu ya Iringa-Mbeya wilaya ya Mufindi.
 
Mwandishi  wetu Diana Bisangao anaripoti kutoka Iringa kuwa akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com ofisini kwake leo Kamanda wa polisi Mkoani Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 22 januari majira ya saa 2 kamili usiku.
 
Kamanda Mungi alilitaja gari hilo aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T.812 CNZ mali ya Elelin Mkombozi mkazi wa Dar es Salaam lililokuwa likiendeshwa na Japhet Maliki(29) ambaye pia ni mkazi wa Dar es Salaam.

Mungi alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa noah, hata hivyo dereva amekamatwa kwa uchunguzi Zaidi.

0 comments: