Mfanyabiashara
wa Kitanzania aliyetambulika kwa jina la Juma Abdallah Kheri ambaye pia
anafahamika kama Chief Abiola au Juma Sahel, alikamatwa siku ya
Alhamisi, Oktoba 31, 2013 mkoani Tanga kufuatia taarifa za kijasusi
zilizomuunganisha na shughuli za kufadhili vitendo vya kigaidi nchini
Tanzania.
Kheri anatuhumiwa kufanya kazi na kukifadhili Kituo cha Vijana wa Kiislamu (MYC), tawi la al-Shabaab nchini Kenya.
Kheri anatuhumiwa kufanya kazi na kukifadhili Kituo cha Vijana wa Kiislamu (MYC), tawi la al-Shabaab nchini Kenya.
"Anashikiliwa
mikononi mwa polisi pamoja na watu wengine wawili na mahojiano
yanaendelea. Kwa hivyo, siwezi kusema zaidi ya hapo sasa," kamanda wa
polisi wa mkoa wa Tanga, Constantine Massawe, amekaririwa akiiambia Sabahi.
Massawe alisema mkoa wa Tanga unaweza kuwa na al-Shabaab kutokana na ukaribu wake na Mombasa, ngome ya MYC.
Massawe alisema mkoa wa Tanga unaweza kuwa na al-Shabaab kutokana na ukaribu wake na Mombasa, ngome ya MYC.
0 comments:
Post a Comment