HABARI KAMILI HII HAPA
Release No. 195
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Novemba 14, 2013
KIM ATEUA 32 KUIKABILI KENYA
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen
ameunda kikosi cha wachezaji 32 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya
kimataifa dhidi ya Kenya (Harambee Stars) itakayochezwa Jumanne, Novemba
19 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi hicho kinajumuisha wachezaji 16
walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na
wengine 16 kutoka Future Taifa Stars. Awali kambi ya Future Taifa Stars
iliyoanza Novemba 9 mwaka huu na kuvunjwa leo asubuhi ilikuwa na
wachezaji 30.
Wachezaji walioitwa ni makipa wanne;
Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Deogratias Munishi (Yanga) na
Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Ismail
Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting),
Nadir Haroub (Yanga) na Said Moradi (Azam).
Viungo wakabaji ni Erasto Nyoni (Azam),
Himid Mao (Azam), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Vincent
Barnabas anayechezea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman
Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo, Hassan Dilunga (Ruvu
Shooting), Jonas Mkude (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Salum
Abubakar (Azam) na William Lucian (Simba).
Viungo washambuliaji ni Faridi Musa
(Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwingi Kazimoto
(Markhiya, Qatar) na Simon Msuva (Yanga).
Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu
Shooting), Juma Liuzio (Mtibwa SugarMbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na
Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC)
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment