WAKATI
leo wajumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha Demokrsia na
maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kalenga wameshiriki katika zoezi la
upigaji wa kura za maoni kuchagua mmoja kati ya wanachama 13
waliojitokeza kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwa wagombea wa
nafasi ya ubunge jimbo la kalenga kupitia chama hicho ,mkurugenzi wa
Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson
Kigaila amesema chama chake kamwe hakitasimamisha mgombea dhaifu
katika kinyang'anyiro hicho na lazima CCM kianze kuzoea kushindwa .
Huku
mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa na mjumbe wa kamati kuu ya
Chadema Bi Chiku Abwao akiwataka wana Kalenga kujenga imani na
Chadema na kuwa haitakuwa tayari kumweka ndugu katika chaguzi hizo
na kuwa CCM imeonyesha kuwadharau wana Kalenga kwa kuendekeza siasa
za familia katika jimbo hilo jambo ambalo halikubaliki.
Akifungua
mkutano huo wa kura za maoni katika ukumbi wa St Dominic mjini
Iringa Kigaila alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kuanzisha
mchakato wa kumpata mgombea wa Chadema na kuwa Chadema ina matumaini
makubwa ya kushinda katika jimbo hilo.
"
CCM walikuwa wakisikilizia ni nani ambae Chadema itamsimamisha
katika jimbo hilo na kuwa walidhani wapo peke yao ila sasa Chadema
inatangaza rasmi kuwa mchakato wa kumpata mgombea wake umeanza
na ni lazima apatikane mgombea ambae atakuwa ni tofauti na mgombea
wa CCM....lazima CCM kwa hapa kilipofika kianze kuzoea kushindwa
katika uchaguzi"
Alisema
kuwa utaratibu wa kumpata mgombea wa Chadema ni utaratibu ambao
hautokani na mtu mmoja ama viongozi pekee wa juu bali ni utaratibu
shirikishi ambao baada ya kutoka katika hatua ya kura za maoni
kitafuata kikao cha kamati ya utendaji ya jimbo kabla ya kamati kuu
ya chama kufanya maamuzi yake Februari 14 jijini Dar es Salaam kwa
kumteua mgombea atakayesimama jimbo hilo la Kalenga.
Hivyo
aliwataka wana Chadema kuwa makini katika kusikiliza kila mgombea
na kuhakikisha wanachagua mgombea ambae atakubalika katika chama
hicho na hata vyama vingine kikiwemo CCM na wananchi wote wa
jimbo la Kalenga.
Kigaila
alisema mchakato wa kuchukua fomu ndani ya chama hicho jumla ya
wana Chadema 16 walijitokeza kuchukua fomu ila hadi juzi siku ya
mwisho kurejesha fomu ni wanachama 13 ndio ambao walirejesha na
kudai kuwa mwitikio huo ni ishara nzuri ya Chadema kuonyesha kukua
zaidi katika jimbo la Kalenga.
Hata
hivyo alisema kuwa Chadema kina imani kubwa ya kushinda kiti
hicho cha jimbo la Kalenga na ushindi huo utakuwa ni mwanzo wa
kukiondoa chama tawala madarakani .
Kwa
upande wake Abwao alisema kuwa CCM kimewasaliti wananchi wa
jimbo la Kalenga kwa kuonyesha kuibeba familia ya aliyekuwa
mbunge wa jimbo hilo Dr Wiliam Mgimwa na kuwaomba wana Kalenga
kuunganisha nguvu zao kumchagua mgombea wa Chadema atakayeteuliwa na
Chama .
Awali
katibu wa Chadema wilaya ya Iringa vijijini Felix Nyondo aliwataja
waliojitokeza kuchukua na kurejesha fomu kuwa ni pamoja na Zubery
Mwachura , Dr Evaristo Mtitu, Akbar Sanga, Grace Tendega, Rehema
Makoga, Sinkala Mwenda, Henry Kavina, Aidan Pungili, Mussa Mdede,
Mchungaji Samweli Nyakunga, Daniel Luvanga, Anicent Sambala na Vitus
Lawa.
Hata
hivyo wagombea 12 ndio waliofika ukumbini hapo huku mgombea
mmoja Zubery Mwachura akikosekana kutokana na kuwa nje ya nchi kwa
shughuli za kikazi.
|
0 comments:
Post a Comment