Kama igizo vile: Mlinda mlango wa Argentina Sergio Romero akiokoa mkwaju wa penati uliopigwa na Ron Vlaar.
KOCHA wa Uholanzi, Louis van Gaal amekiri kuwa wachezaji wawili waligoma kupiga penati ya kwanza baada ya kufungwa kwa penati na Argentina.
Uholanzi walishindwa kurudia kupiga
penati kama walivyofanya katika hatua ya robo fainali dhidi ya Costa
Rica baada ya beki wa Aston Villa Ron Vlaar kukosa penati ya kwanza na Wesley Sneijder naye kukosa.
Argentina walifunga penati zote nne na
kufika fainali ya kombe la dunia ambapo watavaana na Ujerumani kwenye
dimba la Maracana jumapili ya wiki hii.
Baadaye, Van Gaal - ambaye anatarajia
kuanza kazi wiki ijayo katika klabu ya Manchester United - alijitokeza
na kusema kuwa wachezaji wawili waligoma kupiga penati ya kwanza, lakini
hakufafanua zaidi.
Alisema: "Unatakiwa kufunga penati ya kwanza na niliwaomba wachezaji wawili kupiga penati ya kwanza kabla ya kumpata Vlaar.
"Nilidhani kwakuwa alikuwa mchezaji
bora uwanjani angejiamini zaidi. Ilionesha kuwa sio jambo jepesi kufunga
wakati wa mkwaju ya penati".
Kipa wa Argentina, Sergio Romero akiokoa penati ya kiungo wa Uholanzi, Wesley Sneijder.
Dakika 120 za mchezo huo zilimalizika kwa suluhu ya 0-0, lakini Argentina walishinda kwa kufunga penati zote nne.
Van Gaal alishindwa kumuingia kipa
mtaalam wa penati, Tim Krul kama alivyofanya wiki iliyopita kwasababu
alikuwa amemaliza nafasi za wachezaji wa akiba.
Kumuongezea maumivu zaidi, kipa wa Argentina Sergio Romero aliyefanya naye kazi katika klabu ya AZ Alkmaar alidaka penati mbili.
"Hatujapoteza mechi dhidi yao, lakini penati ni mchezo wa bahati". Aliongeza Van Gaal.
"Nilimfunidha Romero jinsi ya kucheza penati enzi hizo tukiwa pamoja, kwakweli inauma".
Mshindi wa mechi: Kipa wa Argentina, Romero akishangilia baada ya kumalizika kwa zoezi la kupiga penati na wao kushinda.
0 comments:
Post a Comment