HOME »
» MKALI WA KOMBE LA DUNIA ASAINI MIAKA MIWILI AZAM FC NA KUSEMA...
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Haiti, Leonel Saint-Preux leo amesaini Mkataba wa miaka
miwili kuichezea Azam FC kuanzia msimu ujao.
Nyota
huyo aliyeicheza Haiti katika Kombe la Mabara ya Dunia la FIFA mwaka
jana nchini Brazil, amesaini mchana huu baada ya kufanya vizuri katika
majaribio ya wiki moja Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
“Nimefurahi
kukamilisha usajili wangu, ni changamoto nyingine nzuri kwangu,
natakiwa sasa kuthibitisha uwezo wangu uwanjani na kutumia uzoefu wangu
wa kucheza mashindano makubwa duniani kuisaidia timu,”amesema.
 |
Nyota wa Haiti Leonel Saint-Preux akisaini Mkataba wa miaka miwili na Azam FC leo Dar es Salaam |
 |
Hapa anakabidhiwa jezi na Meneja wa Azam FC, Jemadari Said |
 |
Wakala wake, Gibby Kalule kushoto akimsaidia kuvaa jezi |
Nyota
huyo aliyewahi kuchezea APR ya Rwanda kwa miezi saba mwaka 2011,
amesema kwamba anaweza kucheza katika mazingira yoyote na hana wasiwasi.
Wakala wake,
Gibby Kalule wa Uganda, amesema ana matumaini mchezaji wake atafanya vizuri Tanzania.
“Nina
wachezaji wengi wazuri ambao watabadili soka ya Tanzania na kuleta
msisimko zaidi, naanza na huyu, atakuwa balozi wangu mzuri
hapa,”amesema.
Meneja
wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari amesema kwamba mchezaji huyo
amemvutia kila mmoja kwa kipindi cha wiki moja alichokuwa na timu, hivyo
wanasubiri kumuona msimu wa mashindano utakapoanza.
Mshambuliaji
huyo aliyezaliwa Machi 12, mwaka 1985 in Cap-Haitien mara ya mwisho
alichezea klabu ya FELDA United F.C. ya Ligi Kuu ya Malaysia.
Kisoka, Saint-Preux alianzia Zenith ya kwao, ambako alikuwa mkali wa mabao katika Ligia ya nchini humo.
Saint-Preux alisaini Minnesota Thunder ya Daraja la Kwanza Marekani Aprili 15, mwaka 2009, kabla ya kuhamia Hanoi ya Vietnam.
 |
Hapa anacheza Kombe la Mabara dhidi ya Hispania |
Machi 2010 alisiani mkataba wa awali na Aztex, lakini akatemwa baada ya kueli vipimo vya afya.
Kimataifa
Saint-Preux, alianzia kuchezea timu za vijana za Haiti wa umri tofauti.
Alikuwemo kwenye kikosi cha Haiti kilichofuzu michezo ya Olimpiki mwaka
2008 mjini Beijing, akifunga bao la kukumbukwa kutoka umbali wa mita 40
timu yake ikishinda 2-1 dhidi ya Canada.
Alianza
kuchezea timu ya wakubwa ya Hati mwaka 2007. Alifunga bao lake la
kwanza timu ya taifa ya Haiti Novemba 19, mwaka 2008 katika sare ya 1-1
Surinam. Haiti ilifungwa 10-0 na Hispania kwenye michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment