TIMU ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boyz’ inacheza mechi ya kujipima nguvu kesho (Julai 11 mwaka huu) dhidi ya Azam U-20 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Mechi hiyo ambayo ni maalumu kwa benchi la ufundi la Serengeti Boyz likiongozwa na kocha Hababuu Ali Omari kuangalia kikosi chao itaanza saa 2 kamili asubuhi. Serengeti Boyz itacheza mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos) siku ya Ijumaa, Julai 18 mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Azam Complex kuanzia saa 10 kamili jioni.
![]() |
Wachezaji wa Serengeti Boys wakiwa mazoezini Uwanja wa Karume |
Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
0 comments:
Post a Comment