
Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, ameamua kuachana na klabu hiyo
baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita aliokuwa akiutumikia klabuni hapo.
Kamwaga aliingia Simba akiwa katibu mkuu
wakati wa utawala wa mwenyekiti Ismail Aden Rage na sasa mkataba wake
umemalizika.
Kamwaga, awali alikuwa msemaji wa klabu hiyo kabla ya mkataba wake
kumalizika mwishoni mwa mwaka jana, ndipo Rage akampandisha cheo na kuwa katibu
mkuu.
Chanzo kutoka ndani ya Klabu ya Simba kilieleza kuwa, katibu huyo amemaliza
muda wake na haijajulikana kama ataongezewa na uongozi mpya au la, lakini
mwenyewe ametoa ufafanuzi na kudai kuwa hataongeza.
“Kamwaga amemaliza mkataba wake aliokuwa akiutumikia chini ya Rage na
haijajulikana kama uongozi uliokupo madarakani utamuongezea mkataba ama la,”
kilisema chanzo hicho.
Kuhusiana na jambo hilo, Kamwaga ambaye kitaaluma ni mwanahabari alikiri
kumaliza mkataba Simba:
“Nimemaliza mkataba wangu na sitaongeza mkataba mwingine.”
Chanzo:Jamvi la Habari
0 comments:
Post a Comment