Mgombea wa
nafasi ya ubunge katika jimbo la Kalenga kupitia CCM; Bw. Godfrey
Mgimwa alipokuwa anatoka baada ya kukamilisha zoezi lake la kurudisha
fomu hiyo.
Mgombea wa
nafasi ya ubunge katika jimbo la Kalenga kupitia CHADEMA; Bi Grace
Tendega alipokuwa anatoka baada ya kukamilisha zoezi lake la kurudisha
fomu hiyo ya ugombea.
Na Riziki Mashaka.
WAGOMBEA
WA NAFASI YA UBUNGE KATIKA JIMBO LA KALENGA KUTOKEA VYAMA VYA CCM NA
CHADEMA WALIPOKUWA WANARUDISHA FOMU HIZO LEO KATIKA UKUMBI WA SIASA NI
KILIMO KATIKA ENEO HILO LA MANISPAA YA IRINGA, MWAKILISHI WA CCM NI
GODFREY WILLIUM MGIMWA NA KUPITIA CHADEMA NI GRACE TENDEGA AMBAO WOTE
WATAANZA KAMPENI ZAO SIKU YA KESHO YA TAREHE 19/02/2014.
![]() | ||
Grace Tendega Mvanda akirudisha fomu kwa Msimamizi wa Uchaguzi Pudenciana Kisika
|
Mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa wa pili kushoto akiwa ameshika bendera ya CCM akielekea kurudisha fomu |
Wana CCm wakimsindikiza Mgombea ubunge wa CCM Kalenga Bw Mgimwa kurejesha fomu leo |
Makada wa Chadema wakimsindikiza mgombea wao jimbo la kalenga leo |
msafara wa mgombea ubunge jimbo la kalenga kupitia Chadema |
MGOMBEA
wa chama cha mapinduzi (CCM) Godfrey Mgimwa na mgombea wa Chama cha
Demokrasia na maendeleo (Chadema) Grace T Mvanda Godfrey Mgimwa
wamerudisha fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Kalenga leo.
Wagombea hao wamerudisha fomu hizo
leo majira ya mchana ambapo mgombea wa Chadema Grace T Mvanda ndie
alikuwa wa kwanza kurejesha akifuatiwa na mgombea wa CCM Bw Mgimwa
Matukio
yote hayo yalifanyika ndani ya ukumbi wa Siasa ni kilimo uliopo
Gangilonga ambapo Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Godfrey Mgimwa
akisindikizwa na wanachama wa CCM alikabidhi fomu ya kugombea ubunge kwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Vijijini Bi Prudenciana Kisaka.
Baada
ya kurudisha fomu Godfrey aliwashukuru wananchi wa Kalenga na wanachama
wa CCM kwa kumteua kuwa mgombea katika chama cha mapinduzi ccm na
kuwaomba wananchi wawe watulivu siku ya uchaguzi na kuwaahidi kuwa
uchaguzi wa Kalenga utakuwa wa amani.
Na
kwa upande wa Katibu wa ccm mkoa wa Iringa Amina Imbo alisema kampeni
zitaanza tarehe 19 februari mpaka tarehe 16 machi ambapo ndo itakuwa
siku ya uchaguzi wa Mbunge wa Kalenga hivyo amewaomba wananchi kukipa
kura chama cha mapinduzi pia amewasihi waandishi wa habari kuandika
habari za haki na zenye ukweli na kuleta amani.
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Iringa Vijijini Bi Delfina
M. Mtavilalo amewashukuru wananchi wa Kalenga na wanachama wa chama cha
mapinduzi kwa kuonyesha ushirikiano wao katika chama na kuwasihi
wasishawishike kwa kuleta vurugu siku ya uchaguzi bali wapige kura kwa
amani na kumchagua mbunge atakayeikwakilisha vizuri jimbo la kalenga.
Huku mgombea wa Chadema Bi Mvanda
akiwahakikishia wanachama wa Chadema na wananchi wa jimbo la Kalenga
kuwa iwapo atashinda katika nafasi hiyo atahakikisha anafanya kazi ya
kuwatumikia wana Kalenga na sio kutafuta heshima ya uongozi.
Kwani alisema kuwa ana uzoefu mkubwa
katika kuongoza na kuwa matatizo ya jimbo la kalenga anayatambua
vema hivyo atahakikisha anatatua kero ya maji , umeme na kilimo
0 comments:
Post a Comment