Tuesday, 11 February 2014

WANACHADEMA 13 WAREJESHA FOMU LEO ZA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA KALENGA NA KESHO KURA ZA MAONI




 Kada wa Chadema na muuza magazeti maarufu mkoa wa Iringa Aidan Pugili kushoto  akirejesha fomu ya  kuomba  kuteuliwa  kuwania  ubunge  jimbo la Kalenga  leo jioni kwa viongozi wa Chadema wilaya ya  Iringa  vijijini kesho  wana Chadema  jimbo la Kalenga  watashiriki kupiga kura za maoni  kuteua mgombea katia  ya wanachama 13  waliojitokeza
 Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa vijijini Felix Nyondo akitangaza majina ya  waliojitokeza  kuchukua fomu leo
 Baadhi ya  wanachama wa Chadema wakiwa  ofisi za  chama  hicho  eneo la Kichangani mjini Iringa
CHAMA  Cha  Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya  Iringa  vijijini  kimepongeza mwitikio mzuri  wa wanachama  wake 13 akiwemo kijana kada na muuza magazeti maarufu  mkoani Iringa Aidan Pungili kwa kujitokeza    kuchukua na kurejesha  fomu  za  kuomba  kuteuliwa  kugombea kumrithi  aliyekuwa  mbunge wa  jimbo la Kalenga marehemu Dr Wiliam Mgimwa 

Katibu  wa   Chadema  wilaya ya  Iringa  vijijini Felix Nyondo  alisema  kuwa  zoezi la  uchukuaji na urejeshaji wa  fomu kwa  wanachama  wake  lilimalizika jana majira ya saa 10 jioni kwa  wanachama  wake  wote  waliojitokeza kuchukua fomu  kurejesha fomu hizo kwa  wakati.

Hata  hivyo  alisema  kuwa  kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa  makada maarufu  waliokuwepo katika vyama mbali mbali  vya  siasa  kikiwemo chama cha mapinduzi (CCM)  kujiunga na Chadema na  kuchukua fomu  za  kuwania nafasi  hiyo ya ubunge jimbo la Kalenga.

Nyondo  alisema  mwitikio  huo ulioonyeshwa na wana  Chadema  jimbo la Kalenga  katika  kujitokeza  kuchukua fomu ni mwanzo mzuri  kwa  Chadema  kumrithi  mbunge  Dr Mgimwa  jimbo  hilo la Kalenga   na  kuwaomba  wana Kalenga kujitokeza  kwa wingi  kumchangua  mgombea wa Chadema mara   katika  uchaguzi mdogo wa  ubunge   jimbo  hilo utakaofanyika  hivi karibuni .

katibu  huyo  alisema kuwa hadi sasa  maandalizi yote kwa ajili ya mkutano  maalum  wa  kura za maoni kwa  wana  Chadema kwa ajili ya kumteua mgombea yamekamilika na (leo) jumatano zoezi hilo  litafanyika kwa  wagombea  waliojitokeza  kupigiwa  kura za maoni.

Aliwataja  waliojitokeza  kuomba  kugombea nafasi hiyo kuwa ni pamoja na Zubery Mwachura , Dr Evaristo Mtitu,Akbar Sanga, Grace Tendega, Rehema Makoga,  Sinkala Mwenda, Henry Kavina, Aidan Pungili, MUssa Mdede, Mchungaji Samweli  Nyakunga,  Daniel *Luvanga,Anicent Sambala na Vitus Lawa .

Kwa  upande  wake Aidan  alisema kuwa anaingia katika mchakato huo kama  haki  yake ya kidemokrasia  pia  kutaka  kuwatumikia  wana kalenga  ambao  siku  zote  wamekuwa  wakikosa kijana wa kuwatumikia zaidi ya  kuwapa  wazee  ambao  wamekuwa  hawawasaidii ipasavyo.

Pia  alisema  wana  kalenga  wanapaswa  kuachana na CCM na badala  yake  kuelekeza  nguvu  zao kwa Chadema ambacho ni chama  pekee  kinachoweza  kuwakomboa  wana kalenga.

Hata   hivyo mvutano  mkubwa  upo kwa  wagombea  hao  ambao karibu wote  wanaonyesha  kuwa na mvuto zaidi kwa wananchi  kutokana na umaarufu  walionao katika  jimbo  hilo la kalenga   .

Katika wagombea hao zaidi ya wagombea  watatu  walipata  kugombea ubunge katika  jimbo  hilo kupitia  CCM na Jahaz Asilia hivyo  kuwa na majina makubwa kwa  wana kalenga wagombea  ambao  ni makada wa CCM ambao  walipohamia Chadema walikifanya chama hicho  kupata  pigo kubwa ni  pamoja na Mwachura ambae alipata kugombea  ubunge jimbo la Iringa mjini mwaka 2010  pamoja na akina  Frederick Mwakalebela na kuamua  kuondoka  CCM baada ya  kuchakachua jina la Mwakalebela , pia Ansent Sambala  alipata kuomba kuwania  ubunge jimbo la Kalenga kupitia CCM kwa zaidi ya mara moja kabla ya  kuhamia   Chadema pamoja na Grace Tendega  ambae  pia  alipata  kugombea ubunge  kupitia Jahaz Asilia katika  jimbo  hilo

Mwisho

Related Posts:

0 comments: