Tuesday, 11 February 2014

LIGI KUU ENGLAND: JUMANNE LEO & JUMATANO USIKU BIGI MECHI ARSENAL v MAN UNITED!!

>>VINARA CHELSEA WAGENI WA WBA!

RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Februari 11
2245 Cardiff v Aston Villa
2245 Hull v Southampton
2245 West Ham v Norwich
2300 West Brom v Chelsea
Jumatano Februari 12
2245 Arsenal v Man United
2245 Everton v Crystal Palace
2245 Man City v Sunderland
2245 Newcastle v Tottenham
2245 Stoke v Swansea
2300 Fulham v Liverpool

BPL2013LOGOLIGI KUU ENGLAND ipo tena Viwanjani Jumanne na Jumatano Usiku kwa Timu zote 20 kucheza na Vinara wa Ligi, Chelsea, wao wako Ugenini huko The Hawthorns Jumanne Usiku kucheza na West Bromwich Albion lakini, bila shaka, Wadau wengi wataisubiri kwa hamu Mechi ya Jumatano Usiku huko Emirates ambako Arsenal, ambao ndio kwanza wametoka kutandikwa Bao 5-1 na Liverpool, watawakaribisha Mabingwa wa England, Manchester United, ambao nao walipokonywa ushindi Dakika ya mwisho baada Fulham kusawazisha na kupata Sare ya Bao 2-2.
Man City, ambao wako Nafasi ya Tatu, baada ya Wikiendi kubanwa kwa Sare ya 0-0 huko Carrow Road walipocheza na Norwich City, Jumatano wako Nyumbani Etihad kuivaa Sunderland ambayo ina kawaida ya kuifunga City kila wakicheza Stadium of Light.
Kwa Arsenal, Mechi hii na Man United ni muhimu hasa baada ya kuchapwa 5-1 na Liverpool na kutolewa kwenye uongozi wa Ligi lakini pia ni mwanzo wa Mechi ngumu ambapo zitafuata Mechi na Tottenham Hotspur, Chelsea, Manchester City na Everton hadi mwanzoni mwa Machi.
Timu zote, Arsenal na Man United, zimekiri matokeo ya Mechi za mwisho ni mabaya kwao na kila mmoja anatafuta afueni kwenye pambano lao.
Mwanzoni mwa Msimu, kwenye Mechi ya kwanza huko Old Trafford, Man United iliifunga Arsenal Bao 1-0 Mfungaji akiwa Robin van Persie ambae ni Nahodha wa zamani wa Arsenal.
Wakati Arsenal bado wako kwenye nafasi nzuri ya kupigania Ubingwa, kwa Man United kuutetea Ubingwa wao sasa ni kitu kigumu mno na iliyobaki ni kusaka kufuzu 4 Bora ili kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Lakini hata hii 4 Bora ni kibarua kigumu kwani wako Nafasi ya 7, Pointi 15 nyuma ya Vinara Chelsea na 9 nyuma ya Liverpool ambayo iko Nafasi ya 4.
Akikiri ugumu wa hali yao, Meneja David Moyes amesema ili wafanikiwe sasa inabidi washinde Mechi zao zote.
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
PTS
GD
1
Chelsea FC
25
17
5
3
47
20
27
56
2
Arsenal FC
25
17
4
4
48
26
22
55
3
Man City
25
17
3
5
68
27
41
54
4
Liverpool
25
15
5
5
63
30
33
50
5
Tottenham
25
14
5
6
32
32
0
47
6
Everton FC
25
12
9
4
37
26
11
45
7
Man United
25
12
5
8
41
31
10
41
8
Newcastle
25
11
4
10
32
34
-2
37
9
Southampton
25
9
9
7
36
29
7
36
10
Swansea
25
7
6
12
32
35
-3
27
11
Hull City
25
7
6
12
25
30
-5
27
12
Aston Villa
25
7
6
12
27
36
-9
27
13
Stoke City
25
6
8
11
26
40
-14
26
14
Crystal Palace
25
8
2
15
18
34
-16
26
15
West Ham
25
6
7
12
26
33
-7
25
16
Norwich City
25
6
7
12
19
37
-18
25
17
Sunderland
25
6
6
13
25
38
-13
24
18
West Brom
25
4
11
10
29
37
-8
23
19
Cardiff City
25
5
6
14
19
44
-25
21
20
Fulham FC
25
6
2
17
24
55
-31
20
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Februari 22
1545 Chelsea v Everton
1800 Arsenal v Sunderland
1800 Cardiff v Hull
1800 Man City v Stoke
1800 West Brom v Fulham
1800 West Ham v Southampton
2030 Crystal Palace v Man United
Jumapili Februari 23
1630 Liverpool v Swansea
1630 Newcastle v Aston Villa
1900 Norwich v Tottenham

Related Posts:

0 comments: