>>LAUDRUP KUISHITAKI SWANSEA KWA KUMTIMUA!
Tuzo hizi hutolewa kila Mwezi na
Wadhamini wa Ligi Kuu England, Kampuni ya Barclays, ambayo pia huteua
Wagombea kwa upande wa Wachezaji.
Kwa Mwezi Januari watakaowania Tuzo ya Mchezaji Bora ni Yaya Toure, Adam Johnson, Santi Cazorla na Luis Suarez.
Kwa upande wa Mameneja, Gus Poyet,
Meneja wa Sunderland, yumo kwenye Listi baada ya kuiongoza Timu yake
kutwaa Pointi 7 katika Mechi 4 baada kuzifunga Fulham 4-1, Stoke, 1-0,
kutoka Sare na 2-2 na Southampton na kufungwa 1-0 na Aston Villa.
Nae Tony Pulis wa Crystal Palace yumo
baada Timu yake kuzifunga Stoke na Hull, Bao 1-0 kila mmoja, kutoka Sare
1-1 na Norwich na kufungwa na Tottenham.
Mourinho aliiongoza Chelsea Mwezi
Januari na kutofungwa baada kushinda Ugenini kwa kuzichapa Southampton
na Hull, kuifunga Man United 3-1 Uwanjani Stamford Bridge na kutoka 0-0
na West Ham.
Manchester City, chini ya Manuel
Pellegrini, walishinda Mechi zao zote 4 kwa kuzifunga Ugenini Swansea,
Newcastle na Tottenham na kuifunga Nyumbani Cardiff City Bao 4-2.
Kwa Wachezaji, Yaya Toure ndie alikuwa ufunguo wa Man City kushinda Mechi zao zote 4 Mwezi Januari.
Adam Johnson wa Sunderland aliweza kufunga Bao 5 ikiwemo Hetitriki walipoichapa Fulham.
Nae Cazorla alikuwa nguzo kwa Arsenal kwa kufunga Bao 3 na mbili zikiwa kwenye ushindi wao wa 2-0 walipoifunga Fulham.
Straika wa Liverpool, Suarez, ambae ni Mfungaji Bora wa Ligi Kuu England, aliifungia Liverpool Bao 4 katika Mwwezi huo Januari.
Suarez na Pellegrini, ikiwa watashinda Tuzo hizi, hii itakuwa mara ya Pili mfululizo kutwaa baada kuzinyakua Mwezi Desemba.
MICHAEL LAUDRUP ATAFAKARI KUISHITAKI SWANSEA BAADA KUMTIMUA!
Michael Laudrup, ambae Jumanne alitimuliwa kama Meneja wa Swansea City, anatafakari kuishitaki Klabu hiyo.
Laudrup alitimuliwa baada ya Swansea
kufungwa Mechi zao 4 kati ya 5 zilizopita na kuwaacha wakiwa Pointi 2 tu
juu ya zile Timu 3 za Mkiani kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England.
Laudrup alitoa Taarifa lake kupitia
Chama cha Mameneja wa Ligi, League Manager's Association (LMA) ambako
amesema atalifikisha mbele suala lake.
Katika Taarifa hiyo, Laudrup alionyesha
kusikitishwa kwake kwa kufukuzwa kupitia Barua fupi ambayo haikueleza ni
kwanini ametimuliwa.
0 comments:
Post a Comment