Jengo la ofisi kuu mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Singida iliyopo mjini Singida.
Na Nathaniel Limu, Singida
MAMLAKA
ya Mapato nchini (TRA) Mkoa wa Singida imewapandisha kizimbani
wafanyabiashara wanne wa mjini Singida kwa makosa mbalimbali, ikiwemo
kutotumia kwa makusudi mashine za kieletroniki (EFD) kukusanyia kodi,
huku wakijua wazi ni kosa kisheria.
Shitaka
lingine linalowakabili wafanyabiashara hao akiwemo Sabra Mohammed na
Khalfani Juma ni kushindwa kulipa kodi ya VAT kwa makusudi, katika
vipindi tofauti tofauti kati ya mwezi februari mwaka jana hadi januari
mwaka huu, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya TRA, kifungu namba 148
cha mwaka 2008.
Mbele
ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya mkoa Singida Joyce Minde, ilidaiwa na
afisa sheria mwandamizi wa TRA kanda ya kaskazini Geva Masele kuwa,
wakati washitakiwa wakiendelea na biashara zao katika eneo la barabara
ya Karume mjini Singida, walifanya makosa hayo na hivyo kuikosesha
serikali mapato.
Hata
hivyo washitakiwa wote walikana mashitaka yao na wapo nje kwa dhamana
ya Sh. Milioni mbili kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja na shauri hilo
litatajwa tena februari 26 mwaka huu.
Wakati
huo huo Robert Mkoma anayefanya biashara zake katika barabara ya
Lumumba mjini Singida, amefikishwa mbele ya hakimu mkazi wilaya Singida
Flora Ndale, kwa shitaka la kushindwa kulipa kodi na kutotumia mashine
ya kietroniki (EFD) kwa makusudi, jambo ambalo ni kosa kisheria.
Ilidaiwa
na afisa sheria mwandamizi wa TRA Kanda ya kaskazini Masele kuwa,
mshitakiwa alifanya makosa hayo kati ya julai mwaka hadi januari mwaka
huu. Hata hivyo mshitakiwa huyo alikana makosa hayo na yupo nje kwa
dhamana ya Sh.Milioni moja hadi februari 26 mwaka huu, kesi yake
itakapotajwa tena.
Katika
shauri lingine, TRA imempandisha kizimbani Rufina Kundya mbele ya
hakimu Asha Mwetindwa wa mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida kwa kosa
la kushindwa kulipa kodi na kutotumia kwa makusudi mashine ya
kieletroniki (EFD), hali ambayo anaikosesha serikali mapato.
Masele
aliieleza mahakama kuwa, mshitakiwa huyo alifanya kosa hilo kati ya
februari mwaka jana hadi januari mwaka huu mjini Singida. Mshitakiwa
huyo naye alikana kosa hilo na yupo nje kwa dhamana ya Sh. Milioni moja
na shauri hilo litatajwa tena siku ya fenruari 27 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment