ASKARI wa vikosi vya Ulinzi na Usalama kisiwani Pemba, wakiutoa mwili wa Marehemu juu ya Mnara wa tangi la Maji Machomanne, ulioangukiwa na ukuta wa tangi hoo
WANANCHI mbali mbali wakiuangalia mnara wa Tangi la Maji Machomanne, ulioanguka na kupoteza maisha ya wananchi watatu leo asubuhi. (picha na Abdi Suleiman
ASKARI wa vikosi vya Ulinzi na Usalama kisiwani Pemba, wakiushusha chini mwili wa marehemu aliyepoteza maisha baada ya kuangukiwa na ukuta wa mnara wa Tangi la Maja Machomanne Pemba
ASKARI wa vikosi vya Ulinzi na Usalama kisiwani Pemba, wakiupeleka mwili wa marehemu katika gari ya kubebea wagonja, ulioelemewa na ukuta wa mnara wa Tangi la Maji Machomanne Pemba
WANANCHI mbali mbali wakiwa katika hospitali ya chake chake , wakitizama miili ya ndugu zao waliopoteza maisha baada ya kuangukiwa na mnara wa tangi la maji Machomanne Pemba
Mkuu wa mkao wa kusini Pemba, Juma Kassim Tindwa, akimfahamisha jambo waziri wa Nnchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, walipofika katika Hospitali ya Chake Chake, kuaangalia majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo.
DAKTARI bingwa kutoka Quba anayefanya kazi zake kisiwani Pemba, (jina halikufahamika) akimtibu mmoja kati ya majeruhi waliolazwa katika hospitali ya chake chake, kufuatia kuwangukiwa na ukuta wa mnara wa tangi la Maji Mchomanne Pemba.
JUMLA ya watu watatu wamefariki ndunia papo hapo na watatu kujeruhiwa baada yakuangukiwa na ukuta mnara wa tangi la maji uliopo machomanne chake chake pemba, majira ya saa tatu za asubuhi ya leo.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Kusini Pemba,
Suleiman Hassan Suleima, amesema kuwa, merehemu hao walifikiwa na mauti
wakiwa katika kazi ya kuteremsha ukuta wa mnara wa tangi la maji ambao
walikuwa wameshaukata.
Kamanda
Suleimana alisema kuwa, ukuta huo ulikuwa tayari umeshafanya ufa wa
kupasuka, hivyo wakati wakiwa kazini kuuteremsha ukuta huo, ulianguka na
kuwaelemea marehemu hao pamoja na mejeruhi waliokuwa juu wakiuteremsha
ukuta huo.
Kamanda
alisema kuwa idadi ya mafundi waliokuwepo kazini hapo, walikuwa ni watu
12 ambapo watatu wamepoteza maisha papo hapo na watatu kujeruhiwa na
kulazwa katika hospitali ya chake chake na wengine sita walikimbia na
jeshi la polisi liko katika utaratibu wa kuwatafuta kwa ajili ya kuelewa
hali zao.
Aliwataja
marehemu hao kuwa, ni Juma Rashid Juma (35)mkaazi wa chanjaani,
Suleiman Mohammed Abdiadi “maarufu golo” (55) mkaazi wa kwale na Salum
Muhidini Vuai “Bandudu” (35) mkaazi Madungu wote ni wakaazi wa wiliya ya chake chake mkoa wa kusini Pemba.
Aliwataja
majeruhi kuwa ni Jakson John (26) mzaliwa wa Iringa mkaazi wa msingini,
Ali Saleh Ali (35) mkaazi wa michakaeni na Yohana Richerd (25) mkaazi
wa machomanne Chake Chake Pemba.
“baada
ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi tulifika katika eneo la tukio na
tukashirikiana kikamilifu na wenzetu wa vikosi vya ulinzi na usalama
wote wa pemba katika kuokoa maisha ya wananchi wetu waliokuwepo
hapo”alisema kaimu kamanda Suleiman.
Aidha aliwataka wananchi kutoa mashirikiano pale panapotokea majanga kama hayo, ili kuweza kuokoa maisha ya wananchi.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, DK Hilali Juma Mohammed, wa Hospitali ya Chake
Chake, amesema kuwa kati ya marehemu hao watatu, wawili waliumia kichwa,
Kifua na Mikono.
Alisema
kuwa merehemu Suleiman Mohammed Abdiadi “maarufu golo” aliumia sehemu
za kichwa ambacho kilikatika moja kwa moja, Kifua na Mikono, hivyo baada
ya kumaliza taratibu za uchunguzi waliweza kuzikabidhi maiti hizo kwa
ndugu na Jamaa zao.
“Tulishirikiana
kikamilifu na vikosi vya ulinzi na usalama vyote pamoja na uongozi wa
Serikali ya Mkoa wa Kusini Pemba, katika kuwakabidhi miili hiyo kwa
jamaa wa marehemu kwa ajili ya Mazishi”alisema Dk Hilali.
Akitoa
tamko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamo wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mhammed, aliwataka wananchi
waliopoteza ndugu zao katika aji ya kuangukiwa na ukuta huo, kuwa na
subra katika kipindi hichi kigumu kwao.
Alisema
kuwa msiba huo, sio wao pekeyao bali ni wataifa kwa ujumla, hivyo
Serikali iko pamoja nao katika msiba huo na itashirikiana nao kwa
mazishi na madawa kwa wale ambao wamepata majeruhi na kulazwa katika
hospitali.
“Nimepokea
habari ya kusikitisha kutoka kwa viongozi wenzangu, kuhusu kuanguka kwa
ukuta na kupelekea kupoteza maisha ya wananchi watatu, na wengine
watatu kujeruhiwa”alisema Mohammed Aboud.
Kwa
upande wake mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, ambae pia ni Mbunge wa
Jimbo la Wawi kisiwani Pemba, Hamad Rashid Mohammed, alisema kuwa
kukosekana kwa taaluma kwa wananchi juu ya vifaa vitakavyo tumika pamoja
na athari zake zitakazo tokea imechangia kutokea kwa tukio hilo.
Alisema
kuwa, hilo lililotokea ni funzo tosha kwa serikali na kuitaka serikali
kuwa makini wakati wote na kabla ya kufanya kitu chochote waangalie
athari yake ili kuweza kuepusha majanga kama hayo.
Aidha
alisema kuwa, kutokea kwa tuki hilo ni funzo kwa tasisi zote za umma
pale wanapotaka kufanya kitu lazima wajuwe athari yake inayoweza kutokea
hapo baadae, ambamba na kuwataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi
hiki kifupi.
“Nawashukuru
sana vikosi vyetu vya Ulinzi licha ya kukosa zana za kisasa, walipopewa
taarifa tu wamefika na kuanza kuokoa maisha ya wananchi, hilo ni jambo
la kuwapongeza, wananchi tuwe pole katika kipindi hiki kigumu cha msimba
kwani ni msiba wetu sote huu.”alisema Hamad Rashid.
Naye
mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Juma Kassim Tindwa, aliwashukuru wananchi
wa maeneo ya Machomanne kwa juhudi zao kubwa walizozionyesha kabla ya
kufika kwa vikosi vya uokozi katika tukio hilo.
Aliwataka
wataalamu wanaotoa tenda kutumia taaluma zao wakati wanapotoa tenda kwa
kuchukuwa wafanya kazi wenyetaaluma, kwa kuangalia wafanyakazi wao
taaluma zao wakati wanapotaka kufanyiwa kazi zao.
Aliwapa
pole familia zote zilizopoteza ndugu na jamaa zao katika eneo la tukio
hilo, katika kipindi hicho kigumu. “ Sina budi kuwapongeza wananchi wote
waliofika katika tukio hilo, na kuweza kusaidia uokozi kabla ya kufika
kwa vikosi vya uokozi katika tukio hili”alisema Tindwa.
Kwa
upande wake Mkuu wa kikosi cha Zimamzoto na Uokozi Pemba, ACF Iddi
Khamis Juma, alisema kuwa katika tuko hilo changamoto kubwa
iliyowakabili ni kukosekana kwa vifaa vya kisasa vya uokozi, hali
iliyopelekea kuchukuwa muda mwingi kwa kutumia vufaa vya kienyeji.
Alisema
kuwa, licha ya kutumika kwa vifaa vya kienyeji lakini waliweza kuziopoa
marehemu zilizokuwa zimekwama katika mnara huo, sambamba na kuwataka
wananchi pindi likitokea tukio kutoa taarifa kwa wakati muafaka kwa
vyombo vya Sheria.
“Tulipopata
taarifa tu tuliweza kupeana taarifa makamanda wote na kufika katika
eneo la tukio na kuweza kuziopoa maiti zilizokuweko juu ya Mnara huo,
ila kikwazo ni zana za uokozi kwani tumetumia dhana duni”alisema.
Naye
mmoja kati ya wafanyakazi katika mnara huo, Said Mohammed , alisema
kuwa katika kazi hiyo jumla wako vijana 12 ambao ndio wanofanya kazi ya
ubomoaji wa mnara huo.
Said
alisema kuwa, wanapofika asumuhi huchonga kuta hilo kwa kutumia drili
ili kuweza kuliangusha au kuvunja kidogo kidogo, na baadae hushuka chini
na kuuvuta kwa gari huo ukuta.
“Leo
kabla ya hawajateremka chini, ukuta uliwaangukia na tukaamua kupanda
juu kwa lengo kuwaokoa merejeruhi kwanza waliokuwepo hapo juu”alisema
kiongozi huo.
Ujenzi huo wa mnara wa tangi la maji Machomanne Chake Chake Pemba, unaendeshwa na kampuni wa Serengeti Limited ya Tanzania Bara.
Na Abdi Sueliman Na Bakari Mussa, Pemba.
0 comments:
Post a Comment