Ili
kuwafikia wananchi wengi, uzinduzi wa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania utakaofanyika kesho, Jumatatu, Juni 3, 2013,
kuanzia saa 8:00 mchana katika viwanja vya Karimjee,
jijini Dar es Salaam utarushwa moja kwa moja na vituo vya TBC1, TBC
Taifa, ITV, Star TV, Channel Ten, ZBC TV na ZBC Redio. Wadau hawa
wamekubali kufanya hivyo baada ya kuombwa.
Uzinduzi huo utarushwa moja kwa moja na vituo hivyo kuanzia saa 8:00 mchana.
Rasimu
hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi
mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo
mikutano, barua pepe, ujumbe mfupi wa simu za mikononi (sms) na
nyinginezo.
0 comments:
Post a Comment