Zikiwa zimebakia takribani wiki 2 kabla ya klabu yake haijapambana na
Arsenal aktika mchezo wa hatua ya mtoano ya michuano ya ligi ya
mabingwa wa ulaya, kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller amesema Arsenal wanacheza
soka safi la kuvutia na kusema timu yao inaelekea katika mchezo dhidi
ya Arsenal wakijua haitokuwa kazi rahisi kuifunga timu hiyo ya Arsene
Wenger.
Arsenal, ambayo walimaliza nafasi ya pili nyuma ya Dortmund katika
hatua ya makundi, watawakaribisha mabingwa watetezi Bayern katika mchezo
wa kwanza wa hatua ya mtoano katika dimba la Emirates mnamo February
19.
Na wakati Muller akiamini vijana wa Wenger wataleta upinzani mkubwa
kwa Bayern, mjerumani huyo pia anaamini utawala wa Bayern katika soka la
ulaya hivi karibuni unaipa nafasi timu yao.
“The Gunners wanacheza soka zuri sana, ndio timu ngumu tuliyopangiwa nayo,; Muller aliiambia Kicker.
“Tuna ubora sawa na timu hii kubwa kutoka kwenye premier league.”
0 comments:
Post a Comment