Standard media Group Kenya imeripoti kuhusu Uhuru wa kuabudu nchini Kenya na jinsi ilivyorahisi kwa yeyote kuanzisha kanisa.
Wanasema uhuru wa kuabudu umesababisha kuenea kwa madhehebu ya kidini
nchini Kenya huku hali ikizidi kuwa mbaya zaidi kutokana na ukweli
kwamba kuanzisha kanisa nchini humo ni rahisi kama kuanzisha kituo cha
misaada.
Ukihitaji kuanzisha kanisa, kinachohitajika ni kujaza fomu, uwe na
katiba na ada ya usajili ya shilingi elfu mbili za Kikenya ambazo ni
zaidi ya elfu 35 za Tanzania.
Baada ya kuwasilisha fomu na ada ya usajili itakulazimu usubiri kwa miezi mitatu na baada ya hapo utaanza kazi ya kanisa lako.
Kwa mujibu wa msajili, sasa hivi nchini Kenya kuna makanisa zaidi ya
10,000 yaliyosajiliwa ambapo kwa upande mwingine, kila siku msajili
anapata maombi zaidi ya 100 ya watu mbalimbali wakitaka kusajili
makanisa yao.
Katika
visa vya makanisa nchini Kenya kuna kimoja nakikumbuka ambacho
kiliripotiwa na NTV kuhusu mchungaji mmoja kumlipa mwanamke aliekua
anajiuza barabarani, yani alimlipa ili akatoe ushuhuda wa uongo
kanisani….
Alichotaka pastor ni umaarufu kwamba anaweza kuombea watu wakapona, watu wakilipata hilo na sadaka zitaongezeka pia…..
0 comments:
Post a Comment