Tuesday, 4 March 2014

`UCHAWI` WA KUWAMALIZA AL AHLY JUMAPILI CAIRO WAANIKWA HADHARANI!!

MMG25849
Na Baraka Mpenja wa  Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
MABINGWA wa soka Tanzania bara na wawakilishi pekee wa nchi katika mashindano ya kimataifa, klabu ya Yanga ya Dar es  salaam imeanza kujifua jana kuelekea katika mechi ya marudiano dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa barani Afrika, klabu ya National Al Ahly ya Misri itakayopigwa mjini Cairo jumapili machi 9 mwaka huu.
Yanga wataingia uwanjani wakiwa na mtaji wa ushindi wa bao 1-0 walioupata katika mchezo wa awali,  uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam machi mosi mwaka huu.
Bao hilo pekee lilifungwa dakika ya 82 kupitia kwa nahodha na beki wake wa kati Nadir Haroub `Canavaro`.
Kuelekea katika mchezo huo, kiungo wa zamani na nahodha wa Yanga, Ali Mayay Tembele amewashauri wana Jangwani kujiandaa vizuri kwani Waarabu wataingia kwa nguvu kubwa kuhitaji kufuta matokeo ya mchezo wa awali. 

Related Posts:

0 comments: