MTU MMMOJA AUAWA MKOANI MBEYA KWA TUHUMA ZA WIZI.
MTU MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 20 – 25
ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUNDI LA
WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI.
TUKIO HILO LILITOKEA MAJIRA YA SAA 04:00HRS HUKO HALENGO JIJI NA MKOA WA MBEYA BAADA YA MAREHEMU KUTUHUMIWA KUIBA KUKU WAPATAO 15 MALI YA EPHRAIM PAUL (37) MKAZI WA NZOVWE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA NA INA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII.
MZEE WA MIAKA70 AUAWA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAGANJO.
MZEE MWENYE UMRI WA MIAKA 70 WENELA
SIBELA. MKAZI WA KIJIJI CHA MAGANJO ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA SHOKA KICHWANI NA KISOGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA VICHAKANI. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 05.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:00HRS ASUBUHI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI WAKATI MAREHEMU AKIWA NJIANI, CHANZO CHA MAUAJI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

MTOTO MWENYE UMRI WA MIEZI 03 AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MOTO.
MTOTO MWENYE UMRI WA MIEZI 03 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA CLARA HONEST AMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MOTO ILIYOTOKEA HUKO ENEO LA BLOCK T MAJIRA YA SAA 11:47HRS ASUBUHI
BAADA YA NYUMBA WALIMOKUWA WANAISHI KUUNGUA MOTO. KIPINDI AJALI HIYO
INATOKEA MTOTO HUYO ALIKUWA AMELALA CHUMBANI WAKATI MAMA YAKE MZAZI
AITWAYE VAILET MAGAVA AKIWA JIKONI ANAPIKA. KATIKA NYUMBA HIYO KULIKUWA NA WAPANGAJI WATANO, KATI YAO WAPANGAJI WAWILI 1. COASTER SIMON (25) MFANYAKAZI WA TBL NA 2. HONEST MARTIN @ SHOO (42)
MFANYAKAZI WA BENKI YA POSTA WALIUNGULIWA VITU MBALIMBALI AMBAVYO
THAMANI YAKE BADO KUFAHAMIKA. MOTO ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO KATI YA
KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI, JESHI LA POLISI NA WANANCHI. CHANZO CHA
MOTO HUO NI HITILAFU YA UMEME. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA KUCHUKUA TAHADHARI ZA MAJANGA YATOKANAYO NA MOTO KWANI YANA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII.
Signed by:
[ROBERT MAYALA - ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment