MTU MMOJA AUAWA KATIKA WILAYA YA MBEYA.
· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA DOLA BANDIA.
· JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU 13 WAKIWA NA BHANGI.
MTU MMOJA AUAWA KATIKA WILAYA YA MBEYA.
MTU MMOJA
ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JAPHET MWANIZUVA (35) MKAZI WA KIJIJI CHA
MWASHIWAWALA ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA MAJIRA YA SAA 06:00HRS ASUBUHI. AWALI MNAMO
TAREHE 01.02.2014 MAJIRA YA SAA 18:26HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MWASHIWAWALA MAREHEMU ALIJERUHIWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI
KICHWANI NA LAITON WILLY. CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI
BAADA YA MTUHUMIWA KUMKUTA MAREHEMU AKIWA NA MKE WAKE SHAMBANI NA
ALISHAWAHI KUMUONYA MARA NYINGI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO
NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANADA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
JESHIO LA
POLISIN MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. SHIDA GIBSON (29) NA
GODFREY MADOKI (32) WOTE WAKAZI WA KISALASI – MAMBA WAKIWA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 3.5. WATU HAO WALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 03.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:30HRS MCHANA KIJIJI CHA KAMABA WILAYA
YA CHUNYA KATIKA MSAKO ULIFANYWA NA JESHI LA POLISI. WATUHUMIWA NI
WAUZAJI NA WATUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAFANYIKA. KAMANADA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA DOLA BANDIA.
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA BRAITH
MUYUTU (38) MKAZI WA CHINGOLA – ZAMBIA AKIWA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA
DOLA BANDIA PAMOJA NA VIPANDE VYA KARATASI [BLACK DOLLAR] NA VIPANDE VYA
MADINI BANDIA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA TAREHE
04.02.2014 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASUBUHI HUKO TUNDUMA KATIKA ENEO LA
MPAKANI KATI YA TANZANIA NA ZAMBIA WILAYA YA MOMBA. TARATIBU ZAIDI ZA
KISHERIA ZINAFANYWA DHIDI YA MTUHUMIWA. KAMANADA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA
WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU/UHALIFU KATIKA JESHI LA POLISI
ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAWASHIKILIA WATU 13 WAKIWA NA BHANGI.
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 13 KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI.
KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA TAREHE 04.02.2014 MAJIRA YA SAA 23:00HRS USIKU
HUKO KATIKA MTAA TAZARA – TUNDUMA KELI BULAYA (46) MKAZI WA MUFULILA –
ZAMBIA AKIWA NA WENZAKE 11 WALIKAMATWA NA ASKRI POLISI WAKIWA NA BHANGI
KETE 226 SAWA NA UZITO KILO 01 NA GRAM 130 PAMOJA NA MICHE YA BHANGI
120. AIDHA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA ENEO LA IGURUSI STENDI YA MABASI
WIALYA YA MBARALI MOSES ANGOMWILE (34) MKAZI WA IGURUSI ALIKAMATWA NA
ASKARI POLISI AKIWA NA BHANGI KETE 47 SAWA NA UZITO WA GRAM 235.
WATUHUMIWA NI WAUZAJI/WATUMIAJI WA BHANGI HIYO. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANADA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KWA
JESHI LA POLISI ZA MTU/WATU WANAOLIMA/KUUZA DAWA ZA KULEVYA ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed by:
[ROBERT MAYALA - ACP]
Kny:KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEAYA.
0 comments:
Post a Comment