MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI.
GARI AMBALO HALIKUWEZA
KUFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA JINA LA DEREVA WAKE LILIMGONGA
MTEMBEA KWA MIGUU MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI KATIKA SHULE YA MSINGI
MBUYUNI ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA DAIMA FAIDA (08) MKAZI WA MBUYUNI NA
KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. AJALI HIYO ILITOKEA MAJIRA YA SAA
06:55HRS ASUBUHI WILAYANI MBARALI MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI HIYO
NI MWENDO KASI, DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU
UMEKABIDHIWA NDUGU KWA AJILI YA MAZISHI. JUHUDI ZA KUMTAFUTA MTUHUMIWA
ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment