KISA WAJUMBE KUGOMA KUCHOMEKEA AJENDA YA KUMTEUA MUME WAKE KUWA MJUMBE
Tumaini Msowoya akiwa na meme wake Frank Kibiki wakati wa harusi yao
Aliyekuwa mwenyekiti UVCCM mkoa wa Iringa Tumain Msowoya
.....................................................................................................................
MWENYEKITI wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa mwanahabari Tumain Msowoya ametishia kujiuzulu nafasi yake hiyo baada ya wajumbe wa baraza kuu la UVCCM mkoa kupinga uamuzi wake wa kuchomoka ajenda ya kumteua mume wake kuziba nafasi tano ambazo anapaswa kuteua kwa mujibu wa kanuni ya UVCCM.
Msowoya alifikia uamuzi huo wa kutangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo jana katika baraza kuu ya UVCCM mkoa lililofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Iringa . Kamujibu wa kanuni ya UVCCM ilipaswa ateue wajumbe watano wa baraza la UVCCM mkoa ambapo wajumbe wanne alikwisha teua katika baraza la vijana lililofanyika Desemba 8 mwaka 2012 hivyo kubaki nafasi moja ambapo jana alipaswa kuiziba nafasi hiyo na kumteua mume wake Frank Kibiki aliyekuwa katibu wa UVCCM Iringa vijijini ambae kwa sasa yupo rikizi. Hata hivyo wajumbe walionyesha kuwa na maswali mengi kuliko majibu ya kuhoji hasa ukizingatia katibu wa wilaya ni mjumbe halali wa baraza kuu la mkoa hivyo hapaswi kuteuliwa nafasi nyingine kuwa mjumbe mara mbili hali wanachama wengine wapo .
Hivyo wajumbe walihoji sababu ya mwenyekiti wao huyo kuingiza ajenda ya uteuzi wa nafasi hiyo moja ambayo mwanzoni haikuwepo katika ajenda za baraza hilo na kumtaka kusubiri baraza lijalo jambo ambalo ajenga hiyo ingeingizwa na si kuchomekea katika baraza hilo.
hatua hiyo ilimfanya mwenyekiti huyo kuingiwa na jazba na hivyo kutangaza kujiuzulu nafasi yake huku akitoka nje ya ukumbi na kupelekea kamati ya utekelezaji ya mkoa kumfuata nje ya ukumbi na kumwolekeza kanuni zinasemaje juu ya uteuzi na namna ya ajenda kujulikana kwa wajumbe na baada ya hapo aliingia ndani ya ukumbi na kurejea kauli yake ya kujiuzulu na kutoka kabisa eneo la mkutano kwa hasira huku akisisitiza kuwa hakushinikizwa na mtu kujiuzulu nafasi hiyo bali ni maamuzi yake binafsi .
Hata hivyo jazba ya mwenyekiti huyo ilitulizwa na wajumbe wa baraza hilo waliopinga uamuzi wake huo.
“Hatukubaliani na uamuzi aliotaka kuuchukua; hawezi kuucha umoja wa vijana katika kipindi hiki ambacho chama kinaelekea kwenye chaguzi ndogo tatu za udiwani mkoani hapa,” alisema mmoja wa wajumbe katika baraza hilo
Aidha mjumbe huyo alisema Msowoya hawezi kujiudhulu nafasi yake hiyo kwa jazba kutokana na kile alichokiita ‘majungu’ yanayopikwa na baadhi ya wajumbe wa baraza hilo. “
Kilichopelekea atishie kujiuzulu ni pamoja na majungu yanayopikwa dhidi yake na baadhi ya wajumbe wa baraza hilo; wengi wa wajumbe hawakubaliani wamekataa azma ya mwenyekiti kutaka kujiuzulu na kuwa kufanya hivyo ni kuonyesha ukomavu mdogo wa kisiasa na sawa na kuwa msaliti ndani ya UVCCM na iwapo wangejua basi wangemchagua mgombea mwingine kata ya waliogombea .
Mwanahabari Tumaini Msowoya alikuwa mwakilishi wa gazeti la Mwananchi mkoani Iringa kabla ya kuhamia gazeti ya Uhuru na Mzalendo mkoa wa Iringa alipata kushinda kwa kishindo kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wa mkoa wa Iringa Oktoba, 2012.
Katika uchaguzi huo, jumla ya kura 302 zilipigwa ambapo Msowoya alipata kura 188 akifuatiwa kwa mbali na mwanahabari Abba Ngilangwa aliyepata kura 76 huku Ramadhani Baraza akiambulia kura 36.
Alipopewa nafasi ya kuwashukuru wajumbe kwa kumpatia ushindi huo, Msowoya alisema anafahamu kazi ngumu aliyoanayo mbele yake ya kuwaangunisha vijana wa mkoa mzima wa Iringa ili kukiletea ushindi chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
“Uongozi unapimwa kwa mambo mengi lakini unapokuwa katika siasa sifa kubwa ni kukisaidia chama chako kupata ushindi,” alisema huku akiomba ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo wanahabari.
Katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Alawi Haidar ametibitisha kutangaza kujiuzulu kwa mwenyekiti huyo japo alisema hadi sasa hajapokea barua rasmi kwa mujibu wa kanuni za UVCCM kutokana na kiongozi anapohitaji kujiuzulu ni lazima kuandika barua .
0 comments:
Post a Comment