>>ENGLAND KUIPINGA MAN CITY YAFUKUTA!!
Kanuni za FFP zimeanza kutumika Msimu
huu baada kuwa na Kipindi cha Mpito cha Miaka Mitatu na, kimsingi,
zinataka Klabu zisitumie Fedha zaidi ya Mapato yao yanayotokana na Haki
za TV, Tiketi Milangoni, Udhamini na Zawadi za Ushindi kwenye
Mashindano.
Ingawa Mfumo huo unaruhusu Madeni kwa
kiwango fulani lakini upo mahsusi kuzuia Matumizi mabovu ya Klabu kwenye
Mishahara ya Wachezaji na Uhamisho wao wakitegemea Ruzuku toka kwa
Wamiliki wao Matajiri.
Akiituhumu PSG, Rummenigge, ambae mbali
ya kuwa Mwenyekiti wa Bayern Munich pia ni Mwenyekiti wa Chama cha
Vilabu huko Ulaya, European Club Association, amesema: “Sifikirii kama
Paris St Germain wanafuata FFP. Sote tunajua Fedha zinazotiririka toka
kwa Wamiliki wao, inadaiwa ni Euro Milioni 200 kwa Msimu. Natumai Rais
wa UEFA, Platini, atafuatilia. Klabu zinazovunja FFP zichukuliwe hatua.
Haiwezekani CHAMPIONZ LIGI iamuliwe na Matajiri toka Urusi au Arabuni! ”
PSG
ilinunuliwa na Wawekezaji kutoka Qatar Mwaka 2011 na kutumia Fedha
nyingi kuwanunua Wachezaji wakubwa kama vile Zlatan Ibrahimovic, Edinson
Cavani na Thiago Silva na Msimu uliopita walitwaa Ubingwa wa France kwa
mara ya kwanza tangu 1994.
Msimu huu wako Pointi 5 mbele kileleni
mwa Ligi 1 na wapo kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI ambapo watakutana na Bayer Leverkusen baadae Mwezi huu.
Huko England kuna minong’ono wapo
Wanasheria wa Vilabu kadhaa ambao wana tafakari kupinga Manchester City
kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao wakitaka Mahesabu yao yachunguzwe
kwa sababu hawaamini kama yanakidhi FFP.
Kitu hiki pia kilidokezwa na Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, Siku kadhaa zilizopita.
0 comments:
Post a Comment