Wednesday, 5 February 2014

VPL: SIMBA YANUSURIKA KWA MTIBWA SUGAR >>SARE YAIPANDISHA SIMBA NAFASI YA 3!

>>COASTAL SARE TENA HUKO MBEYA, ASHANTI YASHINDA!
MATOKEO:
Jumatano Februari 5
Mtibwa Sugar 1 Simba 1
Tanzania Prisons 0 Coastal Union 0
Rhino Rangers 2 JKT Oljoro 2
JKT Ruvu 0 Ashanti United 1

VPL_2013-2014-FPHuko Morogoro, kwenye Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, Simba iliponea chupuchupu kufungwa na Mtibwa Sugar na kulazimisha Sare ya Bao 1-1.
Mtibwa Sugar walitangulia kufunga katika Dakika ya 8 kwa Bao la Mchezaji wa zamani wa Simba, Mussa Hassan Mgosi, na Simba kusawazisha Kipindi cha Pili kwa mashine yao ya Magoli, Amis Tambwe, kufunga Dakika ya 50.
Mtibwa walipata dosari kubwa katika Dakika ya 69 kwa Nahodha wao Shaban Nditi kupewa Kadi Nyekundu na Refa Deonisia Kyura kwa kumkashifu Refa huyo.
Matokeo haya yamewanufaisha kidogo Simba kwa kufungana kwa Pointi na Mbeya City lakini wao kukamata Nafasi ya 3 kwa ubora wa Magoli na sasa wako Pointi 4 nyuma ya Yanga walio Nafasi ya Pili na 5 nyuma ya Vinara Azam FC.
Katika Mechi nyingine za VPL zilizochezwa Leo, huko Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Tanzania Prisons na Coastal Union zilitoka Sare ya 0-0, na Ashanti United ikicheza Ugenini Uwanja wa Azam Complex iliifunga JKT Ruvu Bao 1-0 wakati Rhino Rangers na JKT Oljoro, zikicheza huko Tabora, zilitoka Sare ya Bao 2-2.

MSIMAMO:
NO
TEAMS
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Azam FC
16
10
6
0
29
10
19
36
2
Young Africans
16
10
5
1
34
12
22
35
3
Simba SC
16
8
7
1
33
14
19
31
4
Mbeya City
16
8
7
1
22
13
9
31
5
Mtibwa Sugar
16
5
7
4
20
19
1
22
6
Kagera Sugar
16
5
6
5
15
15
0
21
7
Coastal Union
16
3
10
3
11
8
3
19
8
Ruvu Shootings
14
4
6
4
16
16
0
18
9
JKT Ruvu
15
6
0
9
13
19
-6
18
10
Ashanti United
16
3
4
9
14
28
-14
13
11
Rhino Rangers
16
2
6
8
11
20
-9
12
12
JKT Oljoro
16
2
6
8
12
17
-5
12
13
Tanzania Prisons
14
1
7
6
6
16
-10
10
14
Mgambo JKT
15
2
3
10
7
26
-19
9
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumapili Februari 9
JKT Oljoro v Kagera Sugar
Rhino Rangers v Coastal Union
Mbeya City v Mtibwa Sugar
JKT Ruvu v Ruvu Shooting

Related Posts:

0 comments: