Wednesday, 5 February 2014

WENGER: ‘MBIO ZA UBINGWA ZITAENDA HADI SIKU YA MWISHO!’

 
>>WENGER ATOA UTABIRI WAKE BAADA KUISHUHUDIA CHELSEA IKIIPIGA CITY!
WENGER-INDONESIABOSI wa Arsenal Arsene Wenger anaamini mbio za Ubingwa Msimu huu ziko wazi na zitakwenda hadi Siku ya mwisho ya Msimu.
Wenger alitoa utabiri wake huo baada ya kuishuhudia Chelsea ikiifunga Manchester City Bao 1-0 Jumatatu Usiku huko Etihad, matokeo ambayo yameibakisha Arsenal kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa Pointi 2 mbele ya zote Man City na Chelsea.
Wenger ametamka: “Sio rahisi kama kila Mtu anavyotabiri. Nilisema kitambo hakuna atakaekuwa juu mbali ya wenzake. Hii itaamuliwa na kuwa na matokeo mazuri mfululizo.”
Ingawa Chelsea iliweza kuwa Timu ya kwanza kutofungwa Bao Uwanja wa Etihad wakati Birmingham City ilipoweza kufanya hivyo Novemba 2010, Wenger anaamini matokeo ya Mechi hiyo yangeweza kwenda kokote.
Amesema: “Chelsea walionekana kuwa hatari na City walikuwa wamepooza, hawakuwa wakicheza vizuri na wenye nguvu kama walivyokuwa huko White Hart Lane walipoishinda Tottenham Bao 5 lakini Mechi hii ingeweza kuwa 1-1 na hata Chelsea kushinda 2-0. Mwishoni Chelsea walimiliki Mpira Asilimia 65 na kuwa na Shuti 25 Golini!”
Wenger alieleza: "Kipindi hiki, Januari, Februari, Machi, kila gemu ni vita kwa kila Mtu kwa sababu kila Mtu anapigania kitu. Unataka tu kushinda gemu hizi!
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
24
26
55
2
Man City
24
41
53
3
Chelsea
24
24
53
4
Liverpool
24
29
47
5
Everton
24
12
45
6
Tottenham
24
-1
44
7
Man Utd
24
10
40
8
Newcastle
24
1
37
9
Southampton
24
7
35
10
Aston Villa
24
-7
27
11
Stoke
24
-14
25
12
Swansea
24
-6
24
13
Hull
24
-7
24
14
Sunderland
24
-11
24
15
Norwich
24
-18
24
16
Crystal Palace
24
-18
23
17
West Brom
24
-6
23
18
West Ham
24
-9
22
19
Cardiff
24
-22
21
20
Fulham
24
-31
19
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 8
1545 Liverpool v Arsenal
1800 Aston Villa v West Ham
1800 Chelsea v Newcastle
1800C rystal Palace v West Brom
1800 Norwich v Man City
1800 Southampton v Stoke
1800 Sunderland v Hull
2030 Swansea v Cardiff
Jumapili Februari 9
1630 Tottenham v Everton
1900 Man United v Fulham
Jumanne Februari 11
2245 Cardiff v Aston Villa
2245 Hull v Southampton
2245 West Ham v Norwich
2300 West Brom v Chelsea
Jumatano Februari 12
2245 Arsenal v Man Unitwd
2245 Everton v Crystal Palace
2245 Man City v Sunderland
2245 Newcastle v Tottenham
2245 Stoke v Swansea
2300 Fulham v Liverpool              

Related Posts:

0 comments: