CARROLL AIPONDA FA NA KUDAI NI “FEDHEHA!”
WEST HAM YAKASIRISHWA, ITAAMUA NINI IFANYE!
Carroll alipewa Kadi hiyo kwa kuonekana
na Refa Howard Webb kuwa alimpiga kipepsi Beki wa Swansea Chico Flores
ingawa marudio ya tukio hilo yalionyesha Beki huyo hakupigwa bali
aliparazwa na mkono wa Carroll juu ya kichwa waliporuka wote juu.
Carroll na West Ham walikata Rufaa
kupinga Kadi hiyo na leo FA, Chama cha Soka cha England, kimetoa tamko
kuthibitisha kutupwa kwa Rufaa hiyo huku ikisisitiza uamuzi wa Jopo Huru
ni wa mwisho na hauwezi kukatiwa Rufaa nyingine.
Kwa uamuzi huo, Carroll atafungiwa Mechi
3 na kuzikosa Mechi za West Ham na Aston Villa, huko Villa Park Siku ya
Jumamosi, na zile za Nyumbani Uwanjani Upton Park dhidi ya Norwich na
Southampton.
Wakati Andy Carroll akijibu uamuzi wa
kumfungia Mechi 3 kwa kutoa Posti kwenye Mtandao wa Twitter kwa kuiponda
FA na kuandika: ‘FEDHEHA!’, Klabu yake West Ham inadaiwa kutafakari
nini cha kufanya huku Mtu wa ndani akidaiwa kusema wamesikitishwa na
uamuzi huo ambao Mtu aliehadaa kupigwa usoni, wakati hakupigwa, ndie
mshindi.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 8
1545 Liverpool v Arsenal
1800 Aston Villa v West Ham
1800 Chelsea v Newcastle
1800C rystal Palace v West Brom
1800 Norwich v Man City
1800 Southampton v Stoke
1800 Sunderland v Hull
2030 Swansea v Cardiff
Jumapili Februari 9
1630 Tottenham v Everton
1900 Man United v Fulham
Jumanne Februari 11
2245 Cardiff v Aston Villa
2245 Hull v Southampton
2245 West Ham v Norwich
2300 West Brom v Chelsea
Jumatano Februari 12
2245 Arsenal v Man Unitwd
2245 Everton v Crystal Palace
2245 Man City v Sunderland
2245 Newcastle v Tottenham
2245 Stoke v Swansea
2300 Fulham v Liverpool
0 comments:
Post a Comment