>>KMKM WAPO ETHIOPIA KUIKWAA DEDEBIT!
MABINGWA
wa Tanzania Bara, Yanga, wameingia Kambini huko Bagamoyo ili
kujitayarisha kwa Mechi yao ya Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI
ambayo watacheza na Komorozine de Domoni ya Visiwa vya Comoro Jumamosi
Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Juzi Yanga waliichapa Mbeya City Bao 1-0
kwenye Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom na Jana Wachezaji walipewa
Mapumziko na hii Leo kuingia Kambini kwa ajili ya Mechi hiyo ya Jumamosi
wakiwa chini ya Makocha wao Hans Van der Pluym, Charles Boniface Mkwasa
na Juma Pondamali.
Licha ya wengi kuwachukulia Komorozine
de Domoni, ambao wameshatwaa Ubingwa wa Comoro Mwaka 2010 na 2013, kuwa
ni ‘vibonde’, Charles Boniface Mkwasa amekataa kuwadharau na kudai Soka
la sasa limebadilika na ni bora ujitayarishe vyema.
Mara baada ya Mechi hii ya Jumamosi,
Timu hizi zitarudiana huko Comoro kati ya Februari 14 na 16 na Mshindi
kuingia Raundi ya Kwanza kuwavaa Mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri.
Timu nyingine ya Tanzania ambayo iko
kwenye michuano hii ni KMKM ya Zanzibar ambayo Wikiendi hii itacheza
huko Ethiopia na Dedebit FC na kurudiana Mjini Zanzibar kati ya Februari
14 na 16 na Mshindi kuingia Raundi ya Kwanza kuwavaa CS Sfaxien ya
Tunisia.
CAF CHAMPIONZ LIGI
RATIBA
RAUNDI YA AWALI:
**KUCHEZWA: Mechi ya Kwanza Februari 7-9, Marudiano Februari 14-16
RAUNDI YA KWANZA:
*KUCHEZWA: Mechi ya Kwanza Februari 28-Machi 2, Marudiano Machi 7-9
RAUNDI YA PILI:
**KUCHEZWA: Mechi ya Kwanza Machi 21-23, Marudiano Machi 28-30
TIMU 1 |
Mechi Namba |
TIMU 2 |
Mshindi B |
Mshindi A |
|
Mshindi D |
Mshindi C |
|
Mshindi F |
Mshindi E |
|
Mshindi H |
Mshindi G |
|
Mshindi J |
Mshindi I |
|
Mshindi L |
Mshindi K |
|
Mshindi N |
Mshindi M |
|
Mshindi P |
Mshindi O |
0 comments:
Post a Comment