Wednesday, 5 February 2014

ZIARA 2014: MAN UNITED KUFANYA ZIARA USA KABLA MSIMU UJAO KUANZA!

MAN_UNITED_TOUR_2013Manchester United leo imethibitisha Ziara ya Mwaka 2014, inayodhaminiwa na AON, itafanyika huko Nchini Marekani.
Man United watatembelea Miji kadhaa huko USA ikiwa ni matayarisho yao kwa ajili ya Msimu mpya wa 2014/15.
Hii itakuwa Ziara ya kwanza Marekani tangu watembelee mara mbili mfululizo Mwaka 2010 na 2011.
Ratiba kamili ya Ziara hiyo itatangazwa hapo baadae.
Juzi zilibuka habari kuwa Man United ni miongoni mwa Klabu kubwa 8 za Ulaya zitakazopambana huko Marekani kuanzia Julai 27 hadi Agosti 4 katika Miji 12 kugombea International Champions Cup, Mashindano ambayo yanadhaminiwa na Kampuni ya Guiness.
Vigogo wengine wa Ulaya ni AS Roma, Inter Milan, AC Milan, Real Madrid,  Liverpool, Manchester City na ilitakiwa Juventus wawemo lakini wakajitoa na nafasi yake kujazwa na Olympiakos ya Ugiriki.
Hata hivyo, Man United haijasema lolote kuhusu michuano hiyo na kama pia ipo kwenye Ziara yao hii ya Mwaka 2014 huko USA.
Akiitangaza Ziara hiyo ya Marekani, Mkurugenzi Mtendaji wa Man United, Richard Arnold, alisema: “Nina furaha kutangaza Timu itarudi tena Marekani kwa Ziara ya 2014 inayodhaminiwa na Aon. Tangu Ziara ya mwisho Mwaka 2011, mvuto wa Soka huko Marekani umekua sana. NBC ilitangaza kuwa Msimu huu Ligi Kuu England ina Wastani wa Watazamaji iliyopanda kwa Asilimia 78 toka Msimu wa 2012/13 na Mechi ya Man United na Swansea kuwa ndio Mechi iliyotazamwa na Watu wengi. Man United ina Washabiki zaidi ya Milioni 8 huko USA na hii Ziara ya 2014 ni nafasi kwa Mashabiki hao kuwa karibu na Klabu wanayoipenda.”
Kabla Msimu huu wa 2013/14 kuanza, Man United walifanya Ziara huko Thailand, Australia Japan na Hongkong kwa kuzuru na kucheza Mechi kwenye Miji ya Bangkok, Sydney, Yokohama, Osaka na Hongkong.

0 comments: