Manchester City katika 180 bila goli hata moja.
Timu ya Pellegrini Man City, baada ya kushindwa goli moja kwa bila
nyumbani na timu ya Chelsea Jumatatu iliyopita; Jumamosi hii ilikumbana
na tatizo kubwa la kutoweza kuingiza goli hata moja katika nyavu za
Norwich.
Norwich City iliyokuwa imefungwa magoli saba na Man City katika mechi
ya kwanza, Jumamosi hii waliweka ukuta mkubwa na kufunga milango yao
ili City wasiwaingize goli. Kwa hiyo timu hizi zikatoka sare.
Matarajio yake Pellegrini ya kukalia nafasi ya kwanza yameisha
wikendi hii kwa kuwa wamepinduliwa na klabu ya Chelsea baada ya kuilaza
Newcastle magoli matatu kwa nunge.
Takwimu ya mchezo:
Norwich (4-2-3-1): Ruddy; Martin, Yobo, Bassong, Olsson; Tettey, Johnson, Pilkington (Whittaker 90), Fer, Redmond, Hooper (Van Wolfswinkel 68,).
Wasiotumiwa: Bunn, Hoolahan, Garrido, Becchio, Murphy.
Kadi za manjano: Tettey, Van Wolfswinkel.
Kocha: Chris Hughton
Manchester City (4-4-2): Hart; Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Navas, Milner, Toure, Silva, Jovetic (Dzeko 61), Negredo (Kolarov 77).
Wasiotumiwa: Pantilimon, Richards, Lescott, Rodwell, Lopes.
Kadi ya manjano: Milner.
Kocha: Manuel Pellegrini
Mchezaji hodari: Fer
Refarii: Jon Moss
Mahudhurio: 26,832.
0 comments:
Post a Comment