KIUNGO wa Manchester City Yaya Toure
hatachukuliwa hatua yeyote ya Kinidhamu kwa kosa la kumpiga teke
Mchezaji wa Norwich City, Ricky van Wolfswinkel, wakati Timu zao
zilipotoka Sare 0-0 hapu Jumamosi huko Carrow Road.
FA imethibitisha kuwa Toure hana Kesi ya
kujibu baada ya Jopo Huru la Marefa Watatu wa zamani kulipitia tukio
hilo na kushindwa kuafikiana kwa kauli moja kuwa Toure alipaswa kupewa
Kadi Nyekundu.
Ili FA imfungulie Mashitaka Mchezaji inabidi Jopo hilo limekubaliane wote kwa pamoja.
HABARI ZA AWALI:
MOURINHO ATAKA YAYA TOURE AFUNGIWE!!
>>AKIFUNGIWA KUIKOSA CHELSEA JUMAMOSI!
BOSI wa Chelsea Jose Mourinho amesema Mchezaji wa Manchester City, Yaya Toure, anastahili kufungiwa kwa
kumpiga teke Mchezaji wa Norwich City, Ricky van Wolfswinkel.
Toure, mwenye Miaka 30, anaweza
kufungiwa Mechi 3 kwa tukio hilo liliotokea huko Carrow Road Jumamosi
iliyopita wakati Man City ilipobanwa na kutoka Sare 0-0 na Norwich City.
Akizungumzia tukio hilo, Mourinho
amesema: “Kama hafungiwi basi ujumbe ni wazi: unaweza kufanya lolote.
Kama FA inatetea Soka, basi lazima afungiwe.”
Ikiwa atafungiwa, basi moja ya Mechi
ambazo Toure atazikosa ni ile ya Jumamosi wakati Man City itakapopambana
na Chelsea kwenye Raundi ya Tano ya FA CUP huko Etihad.
FA imesema inangoja Ripoti ya Refa Jon Moss ili itafakari nini cha kufanya.
Akiongelea tukio hilo ambalo Marefa
hawakuliona, Meneja wa Norwich City, Chris Hughton, amekiri: “Hakika
kulikuwa na kitu lakini kama ni Kadi Nyekundu hiyo ni juu ya Refa
kuamua!”
FA CUP
Raundi ya Tano
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 15
1545 Sunderland v Southampton
1800 Cardiff v Wigan
1800 Sheff Wed v Charlton
2015 Man City v Chelsea
Jumapili Februari 16
1630 Everton v Swansea
1800 Sheff Utd v Nottm Forest
1900 Arsenal v Liverpool
Jumatatu Februari 17
2245 Brighton v Hull
0 comments:
Post a Comment