Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ndg. Mbarak Abdulwakil
anatarajia kuzindua rasmi Magereza “Duty Free Shop” – Ruanda, Mbeya
kesho saa 3:30 asbuhi Februari 12, 2014 katika Viwanja vya Ofisi ya
Magereza Mkoa wa Mbeya ambapo shughuli hiyo itashuhudiwa na Viongozi mbalimbali toka Ofisi za Serikali, Binafsi pamoja na Wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya Gereza Kuu Ruanda, Mbeya.
Mpango huu wa ujenzi wa Magereza “Duty Free Shops” katika
Mikoa ya Kimagereza Kiutawala unatekelezwa kwa Mafanikio makubwa na
Uongozi wa Jeshi la Magereza unaosimamiwa kimkakati na Kamishna Jenerali
wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja hivyo kutimiza adhima ya
Serikali ya Awamu ya Nne ya kuwasogezea huduma za bidhaa muhimu na zenye
manufaa Maafisa, Askari wa Jeshi la Magereza pamoja na familia zao
katika maeneo yao ya kazi.
Aidha, mpaka sasa jumla ya “Duty Free Shops” tano (05)
zimezinduliwa sehemu mbalimbali hapa nchini hususani katika Mikoa ya Dar
es Salaam(Ukonga), Dodoma(Gereza Isanga), Morogoro(Chuo cha Ufundi na
Udereva Kingolwira), Kilimanjaro(Gereza Karanga, Moshi) na Mwanza(Gereza
Butimba).
Kuzinduliwa kwa Magereza “Duty Free Shop” – Ruanda, Mbeya
kunafanya idadi yake kuongezeka na kufikia jumla ya Magereza “Duty Free
Shop” sita(06) ambazo zimekamilika hapa Nchini katika Mikoa ya
Kimagereza Kiutawala.
Vyombo vya Habari ikiwa wadau muhimu katika dhima ya
kuuhabarisha umma vinakaribishwa kwenye tukio la uzinduzi rasmi wa
Magereza “Duty Free Shop” – Ruanda, Mbeya kesho Februari 12, 2014
kuanzia saa 3:30 asbuhi katika Viwanja vya Ofisi za Magereza Mkoa wa
Mbeya.
0 comments:
Post a Comment