
Rais
wa chama cha walimu Tanzania(CWT)Gratian Mukoba alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari Feb 7 na miongoni mwa mambo
aliyozungumzia ni pamoja na kero na madai ya walimu kwa serikal
.................................................................................
mwandishi Kenneth John wa matukiodaima.com
Suala la elimu
ni jambo nyeti
sana kwa nchi
yoyote inayohitaji maendeleo
katika Nyanja mbalimbali
za kiuchumi,
kijamii, kisiasa na kibiashara , kwani nchi
yenye nguvu kazi
ya watu wenye
elimu nzuri na
ya kutosha ya ya fani mbalimbali, ni
rahisi pia kwa
nchi husuka kupiga
hatua ya kimaendelea.
Lakini
ni dhahiri kuwa
siku za hivi
karibuni elimu imekuwa
ikishuka kwa kasi
na huku fani
ya ualimu ikizidi
kushuka thamani, kutokana
na sababu mbalimbali
ikiwemo masuala ya
mazingira duni ya
kufanyia kazi kwa
walimu kuanzia makazi
ya kuishi na
vitendea kazi pamoja
na mishahara hafifu
inayoliliwa na
kundi kubwa la
wadau wa elimu mara
kwa mara nchini.
Kwasasa
si jambo la
kushangaza kumsikia mzazi
au mlezi akimweleza
kijana wake kuwa
endapo akifeli katika
mitihani yake atampeleka
kusomea ualimu, na
mara nyingine utawasikia
hata vijana
wenyewe wakiwa katika
maongezi yao
wakisema kuwa mimi
ni kifeli tu
nitaenda kujisomea ualimu ili
nijishikize, hivyo fani
hii inaonekana kama ni
fani ya watu
walioshindwa na kukata
tamaa.
Februari
7 mwaka huu Chama cha
walimu Tanzania kupitia
Rais wa chama
hicho Mwl Gratian
Mukoba, alikutana na
vyombo vya habari
na alibainisha
mambo kadhaa ambayo
yamekuwa yakiendelea kati
ya serikali na
walimu nchini, mambo ambayo
kwa namna moja
au nyingine ukiyaangalia
kwa umakini yanaweza
kuwa yanachangia kudhorotesha
elimu yetu nchini,Miongoni mwa
mambo hayo ni
pamoja na suala
la mishahara duni
na hafifu, suala
ambalo Mukoba katika
taarifa yake kwa
wanahabari alibainisha kwamba
kumekuwa na vikao
mbalimbali vya majadiliano
ya nyongeza ya mishahara kwa
walimu kutokana
na maagizo ya
mahakama kuu ya
Division ya kazi
ya mwaka 2012,Ingwaje
pamoja na vikao
hivyo bado kumekuwa
hakuna chochote kilichopatikana na
badala yake serikali
ilitoa ahadi na
kuwaahidi kuwa ifikapo
februari mwaka huu
majadiliano juu ya
masuala ya kuhusu
nyongeza za mishahara
yatakuwa yamekamilika.
Halikadharika
serikali na walimu
wamekuwa katika mikwaruzano
kuhusiana , na ulipwaji wa
malimbikizo ya madeni
ya mishahara na
yasiyo ya mishahara, ambapo kwa
mujibu wa taarifa
ya februari 7
mwaka huu kutoka
(CWT) ilibainisha kuwa
madai ya walimu
kwa serikali yanayohusiana
na malimbikizo ya
mishahara yanafikia shilingi
Bilioni 40. Sasa
ukitathimini utagundua hali
hii imekuwa ni
miongoni mwa sababu
inayowakatisha tamaa walimu ya kufundisha kwa
moyo, na hivyo
kupelekea viwango vya
elimu kuzidi kushuka
zaidi nchini.
Pamoja
na sababu hizo
lakini pia suala
la upandishwaji wa
madaraja kwa walimu
limekuwa ni suala
linalokatisha tamaa ya
kujiendeleza kielimu kwa
baadhi ya walimu ,ambapo (CWT) katika
taarifa yake ilionekana
kuitupia lawama
serikali kwa kushindwa
kufanya maandalizi mazuri
ya mfumo wa
upandishwaji wa vyeo
kwa walimu yaani (OPRAS).
Hivyo
kutokana na changamoto na kero
hizo za walimu, ni
dhahiri zimekuwa zikiongeza
kusababisha kushuka kwa
viwango vya elimu
nchini,kwani walimu wamekuwa
na changamoto nyingi
mno, ni ukweli kwamba
endapo mazingira ya
kazi na malipo
yangekuwa yakilipwa kwa
wakati husika, na uboreshwaji wa
viwango vya mishahara
ungefanyika kwa vyovyote
vile walimu wangezidi
kujituma kufanya kazi
yao ya kuelimisha
watoto wa kitanzania
vizuri .
Hivyo ni
vyema serikali ikajaribu
kuzitazama changamoto hizo
za walimu kwa
undani zaidi, na
kuzitafutia ufumbuzi
wa haraka ili kuhakikisha
tunaokoa elimu yetu inayozidi
kushuka siku hadi
siku.
Na
ikumbukwe kwamba mara
ya mwisho Chama
cha walimu Tanzania
(CWT) kilipokutana na
vyombo mbalimbali vya
habari nchini, kilitoa
msimamo kuwa endapo
itafika mwisho mwa
mwezi februari hawajapata
ufumbuzi wa kero mbalimbali
zinazowakabilia basi watakuwa
tayari kutangaza mgogoro
na serikali,Hivyo ni vyema kabla
ya kufikia huko,
serikali ikaangalia namna
ya kutatua kero hizo kwani
waungwana husema “Usipoziba
ufa utajenga ukuta”
hivyo ni bora
kushughulikia mapema kero
walizonazo walimu kwa
sasa kabla ya mgogoro
huo kutangazwa mwishoni
mwa mwezi huu ambao
unaweza kupelekea madhara
makubwa zaidi katika
sekta ya elimu
nchini
0 comments:
Post a Comment