MTOTO AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI MKOANI MBEYA.
MTOTO ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA
FRED ROBERT (08) MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI KATIKA SHULE YA MSINGI
MBALIZI NA MKAZI WA MBALIZI ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA
NA PIKIPIKI ISIYOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA DEREVA WAKE. TUKIO
HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 15.02.2014 MAJIRA YA SAA 13:00HRS MCHANA
HUKO MBALIZI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI
WA PIKIPIKI HIYO. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA
KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI
TEULE YA IFISI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI AKAMATWE
NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA SILAHA [PISTOL] BILA KIBALI.
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI 1. JACKSON MWAKALUNGWA (24) NA
2. SAIKO WAILODI (35) DEREVA WOTE WAKAZI WA MLOWO WAKIWA NA SILAHA AINA
YA PISTOL ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI NA INAYOTUMIA RISASI ZA SHOTGUN.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 14.02.2014 MAJIRA YA SAA
14:25HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAHENGE WILAYA YA MBOZI MKOA WA
MBEYA. MTUHUMIWA JACKSON MWAKALUNGWA ALIKAMATWA AKIWA NDANI YA GARI AINA
YA TOYOTA HIACE AKIELEKEA WILAYA YA MBARALI KUFANYA UHALIFU NA ALIKIRI
KUAZIMISHWA SILAHA HIYO NA MTUHUMIWA ALIYEMTAJA KWA JINA LA SAIKO
WAILODI. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA
POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJIMILIKISHA
SILAHA BILA KIBALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA
JAMII KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA
AU PINDI WAONAPO VIASHIRIA VYA WATU KAMA HAO KATIKA MAENEO YAO ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment