Thursday, 6 February 2014

MBUNGE WA IRINGA MJINI MCHUNGAJI MSIGWA AACHIWA KWA DHAMANA


    msigwa d12d5
    Mbunge wa Iringa Mjini Mchg. Peter Msigwa amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Iringa kwa tuhuma za kujeruhi.
    Msigwa anatuhumiwa kutenda kosa hilo juzi kwa kumjeruhi kada wa Chama cha Mapinduzi Salmu Kaita wakati alipokuwa kwenye mikutano ya kampeni ya kumnadi mgombea wa kiti cha udiwani wa Chadema
    Ayub Mwenda inayoendelea katika kata ya Nduli.

    Akisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo Godfrey Isaya,wakili wa serikali Elizaberth Swai alidai kuwa mnamo Februari 5 mwaka huu katika kata ya Nduli mtuhumiwa bila ya kukusudia alimjeruhi Salmu kaita kinyume cha sheria ya nchi sura ya 16 ya mwaka 2002 kifungu cha 225 cha kanuni ya adhabu.
    Hata hivyo Mchg. Msigwa alikana kuhusika na kosa hilo
    Wakili huyo wa serikali aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa shitaka hilo bado haujakamilika na kuomba mahakama kupanga tarehe ya kusikilizwa tena kwa shitaka hilo.

    Mahakama ilikubali ombo hilo lililopangwa kusikilizwa kwa mara ya pili Machi 10 mwaka huu ambapo Hakimu lidai kuwa dhamana ya mtuhumiwa iko wazi kwa kuwa na wadhamini wawili na ahadi ya Sh 2 milioni mashitaka ambayo Msigwa aliyakidhi na kuachiw ahuru.
    Katika kesi hiyo Msigwa alidhaminiwa na Mbunge mwenzake wa viti maalum Chiku Abwao na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Iringa Lilian Msomba.
    Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU wakiwa na mambo ya kutolea amchozi walipiga doria eneo la mahakama huku wakitoa amri ya watu kutokusanyika nje ya viwanja vya mahakama.
    Hata hivyo wafuasi wa Chadema walifurika mahakamani hapo na kuingia katika viwanja vya ndani na kukaa katika makundi.
    Mara baada ya Mchungaji Msigwa kutoka katika chumba cha mahabusi na kupelekwa kizimbani wanachama hao walimzunguka bila ya kuhofia eneo hilo na huku wakionesha vidole viwili juu kama ishara ya salam ya chama chao.
    Baada ya kuachiwa Msigwa wanachama walitoka haraka nje ya jengo la mahakama na kusimama katika viwanja vya nje wakisubiri Mbunge wao atoke katika jengo hilo.
    Msigwa alitoka ndani ya eneo la mahakama akiwa ameongozana na Mbunge mwenzake Chiku Abwao na viongozi waandamizi wa chama hicho wa Kanda ya nyanda za juu kusini , Mkoa wa Iringa na wilaya pamoja na wananchama wao.
    Katika hali iliyowashangaza hata askari wakutuliza ghasi FFU waliokuwa wametanda nje ya viwanja hivyo vya wa mahakama Mchungaji Msigwa alipotoka nje wanachama walimfuata na kumbeba juu juu kisha kuondoka nae.
    Wanachama hao walikuwa wakipokezana huku wakiimba nyimbo za (Chadema Chadema ,Peoples Power,na kufanya maandamano yasiyo rasmi.
    Hata hivyo hatua hiyo iliwalazimu polisi kupanda haraka kwenye magari yao maarufu Defenda na kuanza kufukuzia msafara wa Msigwa ambao ulipitia barabara inayotoke siasa ni kilimo mkabara na bomani na kuunganisha katika barabara kuu ya uhuru.
    Wakiwa karibu na kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani Polisi wakiwa kwenye zile gari mbili walifanikiwa kuzuia maandamano hayo na kumuomba Msigwa kuingia ndani ya gari ombi ambalo baada ya mabishano ya muda mfupi alikubali kuingia ndani ya gari na kwenda moja kwa moja katika ofisi za chama hicho wilaya zilizopo eneo la Mshindo katikati ya mji wa Iringa. Chanzo: Hakimu Mwafongo

    Related Posts:

    0 comments: