Mkuu wa
Polisi Mkoa wa Iringa Kamanda Ramadhan Mungi akitoa nasaha kama sehemu ya
salaam za rambirambi Polisi mkoa wa Iringa. Katika salaam hizo mkuu huyo wa
mkoa amesema jamii inao wajibu kushirikiana na jeshi la polisi katika kupunguza
ajali hizo. Ameelezwa kusikitishwa na baadhi ya abilia kushiriki kumchochea
deleva aende mwendo wa kasi ambao mara nyingi umekuwa ni chanzo kikubwa cha
ajali. Amesisitiza kwamba jeshi la polisi mkoani Iringa litaongeza juhudi zake
katika kupunguza ajali. Akikazia jambo hili Kamanda Mungi alisema “… Leo
tumejumuika nanyi kwa tukio maalumu la kumpoteza askari mwenzetu kwa kifo
kilichosababishwa na ajali usiku wa tarehe 31/01/2014…tumepoteza askari mdogo
sana tuliyemtegemea. Tutakuwa wakali zaidi katika hili kwa sababu taifa
linapoteza sana watu wake kwa njia ya ajali”
Kamanda Mungi
akiwa na waombolezaje wengine….
Mwakilishi wa
Mkuu wa chuo cha mafunzo ya Polisi Moshi Assistant Inspector Castory Chali
alitoa nasaha mara tu baada ya salaam za RPC wa Iringa.
Viongozi
zaidi wa polisi…
Sehemu ya
waombolezaji.
0 comments:
Post a Comment