WA KUFURU ARSENAL, LENGO UBINGWA LIGI KUU MWAKANI
KLABU
ya Arsenal itampa Arsene Wenger Mkataba mono wa Pauni Milioni 24 na day
la pauni Milioni 100 kwa ajili ya kufanya usajili ndani ya saa 72
zijazo, baada ya kumaliza ukame wa mataji wa miaka tisa.
mtandao huu inafahamu Wenger atasaini Mkataba mpya wa miaka mitatu ambao kila mwaka atalipa mshahara wa Pauni Milioni 8.
Na
atapewa bajeti kubwa kihistoria kwa ajili ya kuingia sokoni kufanyia
usajili, ili aiwezeshe Arsenal kutwaa taji la kwanza la ubingwa wa Ligi
Kuu ya England kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004.
Hatimaye:
Arsene Wenger akiwa ameshika kwa madaha Kombe la FA, aliloshinda baada
ya kuifunga Hull City 3-2 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Wembley
Wenger
ameshawishika kuongeza Mkataba baada ya kuiwezesha timu yak kuifunga
Hull City Jumamosi katika fainali ya Kombe la FA - hiyo ikiwa ni mara
ya tank anainua taji hilo akiwa kocha wa Arsenal na sasa atabaki
Emirates.
Alipoulizwa kama Mkataba mpya utasainiwa mapema, alisema: "Ndiyo - kwa sababu ninakwenda Brazil Juni 10,".
Wenger
atapewa Pauni Milioni 100 za kutumia katika dirisha la usajili na
kipaumbele chake ni kuwashawishi beki wa pembeni, Bacary Sagna na keeper
Lukasz Fabianski wabaki katika klabu hiyo, lakini mocha huyo wa pia pia
ametambulisha wachezaji watatu wa kuongeza kuboresha kikosi chake.
Nataka mshambuliaji mpya, kiungo mkabaji, kiungo mchezeshaji na beki wa
kulia.
Muuwaji: Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema (katikati) anabaki kuwa chaguo kuu la for Arsenal
Wachezaji wa Bayern Munich, Mario Mandzukic na wa Real Madrid, Karim Benzema ni miongoni mea wachezaji anaowataka Wenger.
Nyota
wa Bayer Leverkusen, Lars Bender na wa Southampton, Morgan Schneiderlin
ni viungo ambao wamekuwa wakifuatiliwa kwa karibu nawasaka vipaji wa
Gunners, wakati Serge Aurier wa Toulouse, Calum Chambers wa Southampton
na Micah Richards wa Manchester City ni mabeki wa kulia wanaotazamiwa
kuziba pengo la Sagna akiondoka.
Wenger
amesema: "Kwanza inabidi tumsubiri Sagna na kuona atafanya nini - pia
Fabianski. Baada ya halo itabidi tuongeze wachezaji wawili au watatu
kuongeza nguvu kikosini, ni hivyo kwa kweli,".
Mkataba
wa Sagna unamalizika mwezi ujao na atakuwa na mazungumzo na Manchester
City wiki hii juu ya Mkataba wa miaka minne, ambao atalipwa mshahara wa
Pauni 100,000 kwa wiki.
0 comments:
Post a Comment