MAGALACTICO,
Real Madrid wanataka kutumia mbinu zao maarufu za kutangaza ofa nene,
katika kuhakikisha inamnasa mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez na
imesema iko tayari kutoa Pauni Milioni 100 ili kumpata.
Madrid,
ambayo imekosa taji la La Liga na inakabiliwa na mtihani mwingine wa
kumenyana na mabingwa weepy wa Hispania, Atletico Madrid katika fainali
ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wanataka kutumia mbinu zap ki-Galactico kwa
kuanza kuvujisha habari zisizo rasmi juu ya mpoango huo.
Na
magazeti ya kila siku ya michezo Hispania ndiyo yanaonekana kuwa silaha
yao kuu. Lakini inafahamika Madrid inakabiliwa na mtihani mzito kwa
sababu Liverpool haiko tayari kumuuza Suarez na wakati huo huo,
wapinzani wao, Barcelona wanamtaka pia.
Atahamia
Hispania? Luis Suarez anaweza kununuliwa kwa Pauni Milioni 100 na timu
ya timu zinazomuwania, baina ya Barcelona na Real Madrid
Kiwango cha of a ambayo Real inatake kutoa kwa ajili ya Suarez itakuwa rekodi mpya ya dunia na itakuwa vigumu kwa Liverpool kukataa dau hilo.
Licha
ya panda zone kukanusha kwa maana ya mchezaji na klabu yake, lakini
inaaminika kuna kiwango cha dau ambacho kikifikiwa Suarez anaweza kuuzwa
kama atataka kuondoka.
Hilo linatarajiwa kuwa sakata kubwa wakati wa uhamisho wa dirisha kubwa baada ya Fainali za Kombe ka Dunia.
0 comments:
Post a Comment