Wachezaji mashuhuri katika ligi za
soka za Uingereza na zile za Brazil wanajiunga na kampeni ya kuwaonya
mashabiki dhidi ya kuwatumia makahaba watoto wakati wa michuano ya kombe
la dunia nchini Brazil baadaye mwaka huu.
Wachezaji wa kilabu ya Chelsea Frank
Lampard,Oscar na Ramirez wanaunga mkono kampeni hiyo inayoshirikisha
kitengo cha kukabiliana na uhalifu nchini Uingereza pamoja na serikali
ya Brazil.
Kampeni hiyo inawaonya wafuasi wa Uingereza kwamba watakabiliwa na tisho la kushtakiwa iwapo watalipa ili kulala na wasichana walio chini ya umri 18.
Taifa la Brazil linakadiriwa kuwa na nusu ya milioni ya idadi makahaba watoto wanaosimamiwa na na magenge ya uhalifu na kuna hofu kwamba idadi hiyo itaongezeka wakati wa michuano hiyo. Chanzo: bbcswahili

0 comments:
Post a Comment