Wednesday, 12 February 2014

LIVERPOOL YASHINDA 3-2 DHIDI YA FULLHAM NA MAN UNITED NA ARSEANAL WATOA SARE YA 0-0

 Screen Shot 2014-02-13 at 12.41.19 AM
 
Ni mechi ambayo wametoka bila kufungana lakini roho zilikua juujuu kutokana na chupuchupu nyingi zilizotokea kati ya timu zote mbili.


article-2558015-1B6F41AD00000578-648_634x437
 Ni game ambayo Full Time ni Fulham 2 – 3 Liverpool ambapo goli la ushindi la Liverpool limekuja mwishoni kabisa,
Screen Shot 2014-02-13 at 12.46.24 AM Screen Shot 2014-02-13 at 1.06.45 AMScreen Shot 2014-02-13 at 1.08.46 AM

>>MECHI YA MAN CITY v SUNDERLAND YAAHIRISHWA!!
>>EVERTON V PALACE HAIKUCHEZWA!!
>>LIVERPOOL, SPURS ZASHINDA UGENINI!
MATOKEO:
Jumatano Februari 12
Arsenal 0 Man United 0
Everton v Crystal Palace [IMEAHIRISHWA]
Man City v Sunderland [IMEAHIRISHWA]
Newcastle 0 Tottenham 4
Stoke 1 Swansea 1
Fulham 2 Liverpool 3

WAKATI ile Mechi iliyokuwa ikingojewa kwa hamu huko Emirates ikimalizika 0-0 kati ya Arsenal na Manchester United, Mechi za Man City v Sunderland na Everton v Crystal Palace ilibidi ziahirishwe kutokana na hali ya hewa mbaya iliyoambatana na upepo mkali.
Lakini Tottenham, wakicheza Ugenini huko Saint James Park, waliinyuka Newcastle Bao 4-0 kwa Bao mbili za Emmanuel Adebayor, Paulinho na Chadli.
Ushindi huo umezidi kuwaweka Tottenham kwenye Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Liverpool ambao nao walishinda Ugenini huko Craven Cottage kwa kuichapa Timu ya mkiani Fulham Bao 3-2.
Kwenye Mechi hiyo, Fuham walitangulia kufunga baada ya Beki wa Liverpool, Kolo Toure, kujifunga mwenyewe na Daniel Sturridge kusawazisha lakini Fulham walikwenda mbele 2-1 kwa Bao la Richardson na Liverpool kusawazisha kwa Bao la Coutinho.
Huku Matokeo yakiwa 2-2, Refa Phil Dowd aliwapa Liverpool Penati ya Dakika ya 90 baada kuamua Sascha Riether alimchezea Rafu Sturridge na Steven Gerrard kufunga Penati hiyo.
Huko Emirates, Arsenal na Man United zilitoka Sare ya 0-0 Matokeo ambayo yameifanya Arsenal ishindwe kuchukua Nafasi ya Kwanza na kubaki Nafasi ya Pili ikiwa Pointi 1 nyuma ya Chelsea.
Wakitoka kwenye kipondo cha 5-1 walichopewa huko Anfield Jumamosi iliyopita, Arsenal walishindwa kujipa furaha kwenye Mechi iliyokuwa na nafasi chache za kufunga Mabao.
Hii ni Sare ya pili mfululizo kwa Man United baada Jumapili iliyopita kutoka Sare 2-2 na Fulham Uwanjani Old Trafford na wameendelea kukamata Nafasi ya 7 kwenye Ligi.
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs; Arteta, Wilshere; Rosicky, Ozil, Cazorla; Giroud
Akiba: Fabianski, Jenkinson, Monreal, Oxlade-Chamberlain, Podolski, Sanogo, Bendtner.
Manchester United: De Gea, Rafael, Smalling, Vidic, Evra; Valencia, Cleverley, Carrick, Mata; Rooney, van Persie
Akiba: Lindegaard, Buttner, Ferdinand, Fellaini, Young, Hernandez, Januzaj.
Manchester City v Sunderland postponed for safety reasons
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Chelsea
26
17
6
3
48
21
27
57
2
Arsenal
26
17
5
4
48
26
22
56
3
Man City
25
17
3
5
68
27
41
54
4
Liverpool
26
16
5
5
66
32
34
53
5
Tottenham
26
15
5
6
36
32
4
50
6
Everton
25
12
9
4
37
26
11
45
7
Man United
26
12
6
8
41
31
10
42
8
Southampton
25
10
9
7
37
29
8
39
9
Newcastle
26
11
4
11
32
38
-6
37
10
Swansea City
26
7
7
12
33
36
-3
28
11
West Ham
26
7
7
12
28
33
-5
28
12
Aston Villa
26
7
7
12
27
36
-9
28
13
Hull
26
7
6
13
25
31
-6
27
14
Stoke
26
6
9
11
27
41
-14
27
15
Crystal Palace
25
8
2
15
18
34
-16
26
16
Norwich
26
6
7
13
19
39
-20
25
17
West Brom
26
4
12
10
30
38
-8
24
18
Sunderland
25
6
6
13
25
38
-13
24
19
Cardiff
26
5
7
14
19
44
-25
22
20
Fulham
25
6
2
18
26
58
-32
20
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Februari 22
1545 Chelsea v Everton
1800 Arsenal v Sunderland
1800 Cardiff v Hull
1800 Man City v Stoke
1800 West Brom v Fulham
1800 West Ham v Southampton
2030 Crystal Palace v Man United
Jumapili Februari 23
1630 Liverpool v Swansea
1630 Newcastle v Aston Villa
1900 Norwich v Tottenham

Related Posts:

0 comments: