Friday, 8 April 2016

Masanja Mkandamizaji na Wenzako..Vengu Yupo Wapi na Anaendeleaje Kiafya?

Leo Nimesoma Makala moja katika Gazeti fulani wakimuongelea Msanii Vengu Ambae alikuwa Original Comedy kabla ya kuanza kuugua Mwaka 2009 kiasi cha kupelekwa India kupata matibabu, Gazeti hilo wamesimulia jinsi walivyofanya juhudi za kumtafuta kijana huyo ili kujua anaendeleaje baada ya miaka mitano sasa ya ukimya..lakini bila mafanikio hawakuweza kupata lolote la maana kuhusu alipo ama afya yake.....

Masanja na Wenzako wa Original Comedy sisi Washabiki wa Vengu tunataka kujua alipo na hali ya yake kiafya kwa sasa...Tumemmiss.......

0 comments: