Wednesday, 12 February 2014

CHADEMA IRINGA WAMCHAGUA LUCAS SINKALA MWENDA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KALENGA.

 

c24_86467.jpg

Bw. Lucas Sinkala Mwenda amechaguliwa kuiwakilisha CHADEMA katika nafasi ya kugombea ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia kura za maoni zilizopigwa na jumla ya wajumbe 407 wa chama hicho katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa St. Dominic katika manispaa ya Iringa, jumla ya kura 407 zilipigwa na hakuna kura iliyoharibika hivyo mwakilishi huyo amepata jumla ya kura 132 na kufanikiwa kuwapiku wagombea wenzake lakini bado hajapitishwa rasmi kwa kuwa anasubiri maamuzi rasmi kutoka katika kamati kuu ya chama hicho yatakayofanyika tarehe 14/2/2014, hivyo wagombea wote 13 wanatakiwa kuwasili kwenye mkutano wa kamati kuu ya chama utakaofanyika tarehe hiyo, Dar es Salaam.
c23_47c65.jpg
c41_7ec05.jpg
Mkurugenzi mwezeshaji wa mafunzo ya chama hicho Bw. Benson Kigaila akitoa maelekezo na utaratibu kwa wajumbe hao wa CHADEMA kuhusu namna ya upigaji kura na umuhimu wake katika maendeleo ya chama hicho na taifa kiujumla.
c47_92e9c.jpg
Mbunge wa viti maalumu, kupitia chama cha CHADEMA mkoani Iringa, Bi. Chiku Abwao akiongea na wajumbe wa Chadema kwenye mkutano huo wa uchaguzi wa Mbunge atayekiwakilisha chama hicho kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo la Kalenga, mkoani Iringa.
c44_ecfc3.jpg

c50_ff17e.jpg
c49_78279.jpg
Mkutano huo uliudhuriwa na wajumbe wasiopungua 400 kutoka katika pande tofauti za mkoa wa Iringa na jumla ya wajumbe 407 waliwapigia kura viongozi hao na hakuna hata kura moja iliyoharibika,; hali inayoonesha kuitikia wito wa chama.
c38_3b7bc.jpg
baadhi ya wanachama wakiwa wamekaa kwenye vitu mkutanoni hapo.
c12_3d3a3.jpg
c27_163ca.jpg
c31_71fc0.jpg
meza kuu ya viongozi wa CHADEMA wakiwa katika mkutano.
c37_cc8f2.jpg
c48_ea0e9.jpg
c21_bf4b5.jpgc32_781ec.jpgc20_1b3ef.jpg
wagombea wote watakutana na kamati kuu mnamo tarehe 14/2/2014 ili apitishwe mmoja tu pia tarehe 19/2/2014 wagombea wote wawili wataanza kufanya kampeni zao.
Mwandishi, Riziki Mashaka

Related Posts:

0 comments: