Manchester
United imeripoti taarifa ya kuongezeka kwa mapato ya klabu hiyo kwa
11.6% kwa awamu ya pili ya mwaka wa kifedha wa klabu hiyo.
Mabingwa hao wa Barclays Premier League wamesema mapato yao
yameongezeka kutokana ukuaji wa biashara yao ya matangazo na kuuza haki
za matangazo ya TV ya kuonyesha mechi zao.
Mapato ya kuanzia kipindi cha October–December yamekuwa mpaka kufikia kiasi cha £122.9m.
Matangazo ya kibiashara yaliongezeka kwa asilimia 18.8%, wakati
biashara ya kuuza haki za matangazo ya TV kwa ajili ya mechi zao
yalipanda kwa asilimia 18.7%.
Klabu hiyo ilifanikiwa kupata udhamini wa makumpuni sita ya kibiashara.
CEO wa klabu hiyo Ed Woodward alisema kwenye taarifa rasmi: ”Kwa
mara nyingine tena tumeweka rekodi ya kuingiza mapato makubwa kutokana
na mchango mkubwa tunaopata kutoka washirika wetu wa kibiashara, hali
hii inakuja pamoja na kuwa hatufanyi vizuri sana uwanjani, ukiangali
nafasi tunayoshika uwanjani, ni jambo la kusikitisha na kila mmoja wetu
anajua hilo.”
United kwa sasa wanashika nafasi 7 kwenye ligi na wanaweza kukosa
nafasi ya kushiriki kwenye Champions League kwa mara ya kwanza tangu
mwaka 1995.
0 comments:
Post a Comment