KAMBI YA CCM GREEN GUARD, CHIMALA, MBEYA, YAVUJISHA SIRI
Kila kilichokua
kinaendelea katika kambi ya CCM Chimala tulikua na watu wetu. Kamanda Beni wa
mbeya mjini alifanikiwa kuingiza watu kumi;CHADEMA Chimala iliingiza makachero
watatu 3.
Kuna kadi za CHADEMA
200 ambazo zilitoka kwa Braison Mwasimba aliyefukuzwa CHADEMA ( alikuwa katibu
wa tawi CHADEMA Nzovwe, Mbeya) amekabidhi hizo kadi kwa Gunza wa CCM; huyu ni
mwalimu wa Wigamba sekondari (Isanga) na alikuwepo pia katika mafunzo ya Green
Guard Chimala. Kadi hizo za CHADEMA wanapanga kuwapa watu siku ya maazimisho ya
kuzaliwa CCM ili wazirudishe kwa J. Kikwete. Mpango huu mahusui ni kutaka
kumuonyesha Kikwete kuwa CCM inakubalika Mbeya. Hii ni miongoni mwa agenda yao
CCM.
CCM wamewafukuza watu
kumi na tano (15) kutoka kwenye hiyo kambi, ambao nao walikuwa ni “source” wa
hii habari baada ya kupigwa chini. Kati ya walio fukuzwa ni kuwa waligundulika
wanatoa siri na wengine walifanya mgomo kutokana na kuahidiwa malipo ya Tsh
10,000/= kwa siku na badala yake kuwa wanalipwa 2,000/= kwa siku.
Mambo yaliendelea kuwa
mabaya baada ya chakula kuisha kambini. Ndipo mwenyekiti wa CCM wilaya, Ndg
Mathayo Mwangomo alipo amua kumpigia simu mkuu wa magereza wilayani, Rujewa, na
kuomba chakula. Mkuu wa magereza ali mgombeza na kumwambia kuwa usirudie
kunipigia tena simu kwani shughuri za chama na magereza haziingiliani. Baada ya
chakula kuisha ikabidi waanze kutumia pesa ya posho kununua mahindi na viazi.
Hapo ndipo yale malipo ya 2,000/= yakakata na kukawa na mtafaruku
kambini.
Green guard
walianzisha mgomo na kusema kuwa wanafanya mazoezi magumu hawawezi kurishwa
viazi na wanadai fedha zao. Grean gurad waliandamana na kwenda kituo cha polisi
Chimala; walikuwa vijana kama 280. Wakaambiwa waje na viongozi. Baada ya
viongozi kuja wali ongea na kuyamaliza; kesho yake wakapewa 10,000/= kila
mmoja. Kiongozi aliye anzaisha maandamano akapigwa chini, wakati huo vijana
sita washafukuzwa.
Makachero wetu
wamefanikiwa kurekodi maongozi ya makubaliano ya pesa. Pia wamerekodi walivyo
kuwa wanafanya makubariano ya hizo kadi 200 hapo kambini na Ndg Mwasimba.
Wamerekodi hadi maongezi ya kijana walivyo kuwa wakimfukuza na kumnyima nauli;
huyo kijana anatokea Mbeya. Record tuliyo nayo ni audio ambayo itatolewa muda muafaka
utakapo fika.
Kijana mmoja msamalia
mwema wa Chimala ambaye anaitwa Rodi; ni kamanda wa CHADEMA aliwaone huruma
vijana walio fukuzwa na bila kupewa nauli kwani walifukuzwa usiku na hawakuwa
na mahala pa kulala. Alijitolea kuwarudisha mbeya mjini kwa gari lake.
Green Guard imeondoka
leo, Jumamosi, February 1, 2014 kuelekea Mbeya mjini kwaajiri ya sherehe za
kuzaliwa CCM.
On other note; Mathayo
Mwangomo (Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Mbarali) amekuwa akiwatishia watu kuwa
yeye ni serikali na atawaweka ndani. Alikutana na mwenyekiti wa CHADEMA Chimala
ambaye alimchana na kumwambia yeye ni mwenyekiti wa CCM wilaya na sio serikali.
TAKE AWAY: KUNA KADI
ZA CHADEMA 200 ZITARUDISHWA SIKU YA KUZALIWA CCM MBEYA. HIZI NI KADI AMBAZO
ALIYE KUWA KATIBU WA CHADEMA, NZOVYWE , MBEYA, ALIKUWA NAZO. KADI HIZO
HAKUZIREJESHA BAADA YA KUFUKUZWA UONGOZI
0 comments:
Post a Comment