Makocha wanaendelea na maandalizi
kuhakikisha timu zao zimekamilika idara zote ima ni safu ya ushambulizi
,ya kati na safu ya ulinzi kabla ya kipenga cha kuanza kwa kombe la
dunia .
Kulingana na tafiti za ushabiki ,kombe la dunia ndilo lenya ufuasi mkubwa zaidi kote duniani .
Kocha wa Uruguay Oscar Tabarez ,
amesema kuwa washambulizi wa timu hiyo Luis Suarez na Edinson Cavani
wapo katika umri bora wa kushamiri katika kinyanganyiro cha Kombe la
dunia huko Brazil.
Tabarez anamatumaini kuwa kuwa
washambulizi wake wanaujuzi na uwezo wa kutwaa kombe hilo baada ya
kufuzu kwenye hatua ya nusu fainali katika kombe la duna la 2010.
Uruguay ambayo imewahi kushinda kombe
hilo mara mbili iko katika kundi D na Costa Rica, Uingereza, Italia na
wenyeji Brazil. Chanzo: bbcswahili
0 comments:
Post a Comment